Tusiwe Sehemu ya Matumizi ya Nguvu wakati wa Uchaguzi.

Askari wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wametakiwa kutokuwa chanzo cha Matumizi ya Nguvu wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utakaofanyika Mwezi huu huku wakitakiwa kufuata Sheria za Ukamataji Salama walizofundishwa na Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Longido Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Tausi Mbalamwezi wakati akitoa elimu hiyo kwa askari wa Jeshi la akiba ambapo amewataka kuzingatia Sheria na miongozo ya Uchaguzi iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi.

ASP Mbalamwezi ameongeza kuwa endapo mazingira ya uvunjifunzi wa amani ya tatokea zipo taratibu ambazo zitawaongoza katika kutekeleza majukum yao.

Amesisitiza kuwa askari ni kimbilio la wengi katika changamoto ndani ya jamii ambapo amewataka askari hao kuendeleza imani hiyo kwa jamii.

Related Posts