Dk. Slaa Aachiwa Huru, Kesi Yake Yafutwa – Global Publishers



Kutoka katika Mahakama ya Hakimu ya Mkazi Kisutu jijini Dar ni kwamba mahakama imemuachia huru Dk Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Shauri Na.993 la mwaka 2025 Dk Slaa alishtakiwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wa X ambapo leo Februari 27, 2025 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema amewasilisha shauri hilo ya kuwa DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi Franco Kiswaga.

Wakili Mrema ameeleza mahakamani hapo kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania mwenye umri wa miaka 76 ameachiwa huru leo.


Related Posts