Na Oscar Assenga,Pangani.
RAIS DKt Samia Suluhu amesema kwamba Serikali inakusudia kujenga Kiwanda Kikubwa cha Sukari eneo la Bandarini Jijini Tanga ili kujitosheleza na mahitaji hapa nchini.
Aliyasema hayo February 26,2025 mjini Pangani wakati wa ziara yake ya Wilayani Pangani baada ya kuweka jiwe la Msingi Kwenye barabara ya Tanga-Pangani pamoja na daraja la Mto Pangani ambalo litakuwa mkombozi Mkubwa Kwa wananchi.
Alisema Kwa sababu malighafi ya kiwanda hicho itatokea wilaya ya Pangani kutokana na kwamba wilaya hiyo inakwenda kubadilika kutokana na wanakwenda kuja na kilimo kikubwa cha Miwa ndani ya wilaya hiyo.
“Pangani inabadilika na itaendelea kubadilika kwa sababu tunakwenda kuja na kilimo kikubwa cha miwa ndani ya Pangani na Kiwanda cha sukari na tunajenga Tanga Jiji”Alisema Rais Dkt Samia Suluhu
” Tunajenga Viwanda vingi vya sukari ili kujitosheleza mahitaji yetu na kuweza kuhifadhi sukari na kiwanda hicho kitajengwa karibu na Bandari ya Tanga na Shamba litakuwa Pangani na kufungua fursa za ajira za Tanga”Alisema.