Mzize, Ateba waibeba Dabi ya Kariakoo

MWISHO wa ubishi. Wakati pambano la Dabi ya Kariakoo likipigwa leo Jumamosi, huku kila upande ukitamba na washambuliaji wenye uchu mkubwa wa kufumania nyavu, Simba ikiwa na Leonel Ateba, Jean Ahoua na Steven Mukwala, wakati Yanga ina Clement Mzize, Prince Dube na Pacome Zouzoua.

Pambano hilo linalopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:15 usiku timu zote zitashuka uwanjani zikiringia ubora wa vikosi na hususani eneo la mbele ambalo limekuwa likigawa dozi za maana kwa wapinzani, huku Yanga wakiwa bora zaidi kulinganisha na watani wao.

Hili ni pambano la marudiano la duru la pili, baada ya awali kuvaana duru la kwanza Oktoba 19 mwaka jana na Yanga kushinda kwa bao 1-0 lililotokana na beki wa Simba Kelvin Kijili kujifunga katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Maxi Nzengeli.

Ili timu ipate ushindi hatua ya kwanza huangaliwa makali ya safu yake ya ushambuliaji, ambayo ni mahususi kwa kufunga ingawa miaka ya sasa klabu zinaweza kupata mafanikio kutokana na ubora wa viungo wake na idara zingine.

Yanga na Simba nazo zinahesabu zake kulingana na safu zao za ushambuliaji, kwa namna zilivyo kwenye ubora, huku wenyeji wa mchezo huo ambao pia ni vinara wa msimamo wa ligi, takwimu bora zinaonekana kuwabeba.

Msimu huu timu hizo mbili kila moja imekuwa na ubora wake kwenye safu ya ushambuliaji, zikijigawanya kwenye makundi tofauti, lakini Yanga imejiweka kwenye ubora zaidi kabla ya kwenda kukutana na Simba wikiendi hii.

WN 01

Mzize ambaye huu ni msimu wake watatu Yanga, akionyesha uhatari wake kwa kuongeza rekodi yake ya mabao kila msimu.

Msimu huu hadi sasa amefunga mabao 10, asisti tatu, Ni miongoni mwa mastaa watakaowasumbua mabeki wa Simba kutokana na uwezo wake wa kupiga mashuti ya mbali, lakini hari ya kucheza anapokuwa uwanjani.

Alikuwa mshambuliaji pekee aliyetoa asisti mbili katika mchezo wa dabi msimu uliopita ambao Yanga ilifunga mabao 5-1.

WN 02

Ubao wake wa rekodi unasoma vyema akiwa na mabao 10 na asisti 07, huu ukiwa msimu wake wa kwanza Yanga, akitokea Azam FC.

Tangu atue Yanga hajaweka rekodi ya kuifunga Simba, ila Wekundu hao wanamkumbuka katika mechi za Mzizima Dabi alivyokuwa mshambuliaji hatari kwao.

Mabeki wa kati wa Simba, Dube alishawahi kukutana nao, hivyo kama atapewa nafasi ya kucheza basi watakuwa na kazi ya ziada ili rekodi zisijirudie.

WN 03

Msimu wa tatu Yanga akiwa amecheza dabi tisa, akikumbukwa msimu uliopita alipoifungua mlango wa mabao dakika ya 03 kipindi cha kwanza katika mchezo uliochezwa Novemba 5, 2023.

Ni mshambuliaji mzuri ila mara nyingi anaanzia benchi, japokuwa msimu huu hajacheza mechi nyingi ila amefunga mabao 3  na asisti 1.

WN 04

Mshambuliaji mpya wa Simba ambaye amesajiliwa msimu, ni mzuri wa kutumia nafasi na mwepesi wa kutengeneza mazingira ya penati ambayo yamekuwa yakikinufaisha kikosi hicho.

Amekuwa mshambuliaji kinara, ambaye anapata nafasi ya kucheza muda mwingi kikosi cha kwanza, hivyo huenda Kocha Fadlu Davids akaanza nae.

Rekodi zake nazo sio mbaya kwani katika mabao 46 iliyofunga Simba, yeye ameshiriki nane bila kutoa asisti hata moja, huku akiwa amecheza dabi mbili akiwa hajaifunga Yanga.

WN 05

Mshambuliaji Steven Mukwala raia wa Uganda amejiunga na Simba na kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoka Asante Kotoko ya Ghana.

Mukwala mwenye umri wa miaka 24 ni mshambuliaji kinara akiwa na mabao nane na asisti mbili, huwezi kubeza uwezo wake wa kufunga na kutengeneza nafasi, amekuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo.

Mabeki wa Yanga Dickson Job na Ibrahim Bacca wanakazi ya ziada kutokana na uwezo mkubwa wa kutumia nafasi na kufunga alionao.

WN 06

Mshambuliaji kinda na Mzawa ambaye amesajiliwa msimu huu, hajawahi kukutana na joto la dabi kabisa, licha ya kufunga mabao mawili bila asisti.

Kutokana na rekodi zake anaweza asicheze au akaingia dakika za mwishoni kwani kocha amekuwa akicheza kutokea benchi muda mwingi.

Kirekodi washambuliaji wa Yanga wako vizuri ila huwezi kuwabeza pia wa upande wa Simba kwani wamepishana kwa wastani wa mabao mawili tu.

Hivyo mabeki wa pande zote mbili ambao ni Kapombe, Che Malone Fondoh,Abdulrazack Hamza,Mohamed Hussein, David Kameta,Valentine Nouma (Simba), huku kwa Yanga ni Ibrahim Bacca, Chadrack Boka, Kibwana Shomari, Israel Mwenda, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

Yote kwa yote ni kwamba pambano la leo licha ya kuangaliwa sana eneo la viungo, lakini kule mbele Mzize na Ateba au yeyote kati ya washambuliaji wa timu hizo wataiamua mechi hii ya 114 ya Ligi ya Bara tangu 1965.

Related Posts