Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeendesha mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni mpya za mwaka 2024 kwa watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo jengo la 3 la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere na kuwapatia vyeti watumishi wapatoa 84 waliohudhuria mafunzo hayo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo amewashukuru watoa mafunzo kutoka PSPTB kwa kuratibu mafunzo hayo yanayoenda kuwapa kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.
Pia Mombokale ili kusaidia idara ya Ununuzi wawapo katika majukumu yao amedhamiria kuwekeza kwenye idara tumizi kwa kuwapa mafunzo ua usimamizi wa mikataba ya Ununuzi ili kuleta ufahamu Zaidi wanapokwenda kusimamia miradi mbalimbali ya taasisi.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma kutoka Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Amos Kazinza amesema Bodi hiyo imetoa mafunzo ya Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi kwa kuzingatia sharia ya ununuzi ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni mpya za mwaka 2024 ambapo mafunzo haya yamehusisha wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wa TAA kutoka kwenye kanda zao, makao makuu pamoja na wajumbe wa Bodi ya Zabuni ili kupata uelewa wa namna nzuri ya kufanya manunuzi katika Mamlaka hiyo.
Kazinza amesema sharia hii imekuwa na mabadiriko mengi ya sharia mpya mbapo inawataka wajumbe Bodi ya Zabuni waweze kuidhinisha baadhi ya manunuzi kulingana na ukomo wa uidhinishaji lakini pia mhasibu naye anaowajibu wa kuidhinisha manunuzi kulingana na ukomo wa udhinishaji pamoja na wataalamu wa ununuzi na ugavi ambao sasa wamekuwa na jukumu ka ugavi ambalo lilikuwa kwenye sharia ya fedha nayo imeletwa kwenye sharia mpya kwaiyo wataalamu wanayo majukumu ya ununuzi pamoja na majukumu ya ugavi ili kuhakikisha myororo wa ugavi unasimamiwa vizuri.
“PSPTB inaowajibu wa kuhakikisha kwamba wadau wote wanaosimamia ununuzi na ugavi wanapata uelewa wa pamoja ili kuhakikisha dhamani ya fedha inapatikana kwa kila mradi ambao unatekelezwa na taasisi au mamlaka” amesema Kazinza
Kazinza ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi ya kuona fursa hii ya kuwajengea uwezo wataalamu wao kwasababu ya sehemu kubwa ya matumizi ni ununuzi.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma kutoka PSPTB Amos Kazinza akizungumza namna Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ilivyodhamilia kuwafikia wataalamu wao ili kutoa mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni mpya za mwaka 2024
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo akikabidhi vyeti kwa baadhi ya washiri wa mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni mpya za mwaka 2024 yaliyokuwa yanatolewa na PSPTB.
Baadhi ya washiri wa mafunzo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo alipokuwa anafunga mafunzo ya sheria mpya ya ununuzi wa umma ya mwaka 2023 na kanuni mpya za mwaka 2024 yaliyokuwa yanatolewa na PSPTB