KIJANA Khamis Luwoga (45) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Hukumu hiyo imesomwa leo Februari 26,2025 na Jaji Hamidu Mwanga Wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamuhuri ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo.