Pamba yakwepa mtego wa Yanga

DOZI nene zinazoendelea kutolewa na Yanga katika mechi za Ligi Kuu Bara zimelishtua benchi la ufundi la Pamba Jiji ambalo limetangaza kujipanga mapema kukwepa mtego huo kwa kuzungumza mapema na wachezaji kuhakikisha hawaingii wanmaepuka kupigwa nyingi wakiwa nyumbani.

Pamba kesho Ijumaa inatarajiwa kuwa wenyeji wa mchezo huo wa raundi ya 22 utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa, huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 4-0 ilichopewa katika mchezo wa kwanza uliopigwa mwaka jana kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ushindi huo wa Yanga katika mchezo huo uliopigwa Oktoba 3, mwaka uliotokana na mabao ya Ibrahim Bacca, Stephane Aziz KI, Maxi Nzengeli na Kennedy Musonda, ilisababisha aliyekuwa kocha wa Pamba kipindi hicho, Goran Kopunovic kutimuliwa na kuletwa Fred Felix ‘Minziro’. Kipigo hicho kilikuwa cha kwanza kwa Pamba iliyopanda daraja msimu huu sambamba na KenGold, lakini kilikuwa cha pili katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kile ilichopewa Fountain Gate kutoka kwa Simba.

Kutokana na hali hiyo na namna Yanga imekuwa ikigawa dozi katika mechi tatu kati ya tano zilizopita ilipozishindilia KMC na KenGold mabao 6-1 kila mmoja kabla ya majuzi kuifunga Mashujaa 5-0, kwatai Pamba imetoka kupata sare ya 2-2 na Singida BS baada ya awali kufungwa 2-0 na Mashujaa iliyokata wimbi la ushindi wa mechi tatu mfululizo ilizocheza timu hiyo, benchi la ufundi la Pamba limeshutuka.

Kocha Msaidizi wa Pamba, Mathias Wandiba ‘Master’ alisema kuwa wanajua ubora wa Yanga katika eneo la ushambuliaji lakini pia wanatambua madhaifu yao huku akitamba kuwa wana wachezaji bora wenye uwezo wa kuimudu Yanga na kuvuna alama tatu nyumbani.

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo tunajua wana ubora wao mzuri kwenye eneo lao la mbele hilo tumelichukua lakini wana udhaifu wao kwahiyo tutatumia mazuri yao kuyatengeneza yawe dhaifu kwao ili yale mazuri yao yote kama unavyoona tunaendelea na mazoezi yetu tunayafanyia kazi hizi siku mbili,” alisema Wandiba n kuongeza;

“Tunawaandaa wachezaji wetu hasa katika nafasi ya ulinzi naamini kila kitu kitawezekana tumeshajua ni kitu gani tunakwenda kukifanya, niwatoe shaka kwamba tunakwenda kucheza mechi ambayo tutawapa Yanga mchezo mzuri ili tubakie na pointi tatu katika uwanja wetu wa nyumbani.”

Mshambuliaji wa Pamba, Habib Kyombo morali ya timu iko juu wachezaji wana hamu ya mechi, hivyo utakuwa mchezo mzuri huku akitoa tahadhari kuwa lazima waiheshimu Yanga ni timu kubwa lakini Pamba nayo ina wachezaji wazuri, wakubwa na wenye uzoefu na kuahidi kutowaangusha mashabiki wao.

Kiungo mshambuliaji, Salehe Masoud alisema; “Mashabiki watarajie kama tulivyomfanya Azam kwa sababu mtu anaweza kudharau lakini timu yetu ni nzuri kama wanadhani watatoka Dar es Salaam kuja Mwanza kuchukua pointi tatu, waondoe hicho kitu.”

Huku kipa wa Pamba, Yona Amosi alisema maandalizi ya mchezo huo yapo kama ilivyo kwa mechi nyingine na kwamba hakuna ugumu wowote kuikabili Yanga kwani benchi la ufundi linapambana kuwaandaa vyema ili kushinda mchezo huo na kuendeleza wimbi la ushindi katika uwanja wa nyumbani.

v Tabora United (nyumbani)

v Fountain Gate (nyumbani)

v JKT Tanzania (nyumbani)

Related Posts