Muhimbili yapokea mashine ya uchunguzi saratani ya matiti

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) imepokea mashine maalumu Mammography aina ya Senographe Pristina 3D yenye thamani ya milioni 800 kwa ajili ya kufanya uchuguzi wa saratani ya matiti.

Pia machine hiyo itatumika katika kuwafundishia wataalam na kufanya tafiti mbalimbali.

Akizungumza katika hafla ya kupokea mashine hiyo leo Aprili 17, 2024 Dk.Hamad Nyembea wakati akimuwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema takwimu za kidunia zinaonyesha wanawake Milioni 2.3 wanagundulika kuwa na saratani ya matiti kila mwaka.

“Tafiti za kidunia zinaonyesha wanawake milioni 2.3 wanagundulika na saratani ya matiti kila mwaka lakini hapa nchini wanawake 42,000 kila mwaka wanagundulika na saratani hiyo huku wanaofika kwenye vituo vya afya kupata matibabu ni asilimia 38 tu”,amesema Nyembea.

Amesema ujio wa mashine hiyo inaonyesha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Marekani na kuwezesha kukuwa kwa teknolojia katika sekta ya afya.

Dk.Nyembea aliendelea kueleza kuwa saratani ambayo kwa sasa inaisumbua nchi ni saratani ya shingo ya kizazi na tayari jitahada zinaendelea kufanyika ila kuhakikisha saratani hiyo inaisha nchini.

Pia amepongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika sekta hiyo huku akitoa rai kwa watendaji kuhakikisha wanaitunza mashine hiyo na kuhakikisha inafanya kazi iliyokusudiwa.

Ametoa wito wanawake kuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti ili waweze kupata tiba ya haraka pindi wanapogundulika na tatizo hilo kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Taifa ya Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema hiyo wamepokea kwa ukarimu wa Serikali ya Marekani kupitia Jumuiya ya Radiorojia ya Amerika Kaskazini (RSNA )na GE health care .

Amesema mashine hiyo ni ya kisasa zaidi yenye thamani ya milioni 800 na ya kwanza ya aina yake kusimikwa katika hospitali ya muhimbili na inauwezo wa kufanya kazi huduma za kichuguzi za kawaida na kibobezi za matiti.

“Saratani ya matiti ni tatizo kubwa sana nchini Tanzania ambapo takwimu zinaonesha kuwa hii ni saratani ya pili Kwa wanawake katika nchi yetu na inaendelea kuongezeka inawezekana ugonjwa huu kudhibitika na kutibika kabisa ikiwa ugunduzi wake utafanyika mapema,” amesema Profesa Janabi.

Amesema bado kuna chagamoto kubwa ya wagonjwa wapya wa saratani kufika hospitali ambapo kila mwaka inakadiliwa ni asilimia 38 tu ya wagonjwa wapya ndio ufika hospital Kwa matibabu.

Amesema kupitia mashine hiyo itawezekana kufanya utambuzi wa mapema na kuokoa maisha ya wanawake wengi.

“Hospitali ya Muhimbili ni mwanga wa matumani Kwa wengi tunakadilia walau si chini ya wagonjwa 2000 au 2400 kwa mwaka wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja kwa kupimwa na machine hii ya kisasa Pristima 3D.

Naye Mwakilishi wa kitengo cha biashara kutoka GE healthcare Guillaume Fusari amesema ukosefu wa elimu kuhusu saratani ya matiti ndio unapelekea ongezeko la ugonjwa huo ambapo unapelekea vifo hivyo ni muhimu kuwawezesha wanawake ili kupunguza idadi ya vifo.

“Ukosefu wa elimu ndio sababu ya wanawake kuugua ugonjwa huu wa saratani ndio maana kuna umuhimu wa kuwawezesha wanawake ni muhimu ili kuboresha kiwango cha vifo,”amesema Fusari.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *