KOCHA Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema hakuna mechi rahisi ya dabi wanawaheshimu wapinzani wao kutokana na kuwa bora lakini wao pia wamejiandaa kukabiliana nao.
Matola amesema mchezo wa kesho ni mchezo tofauti na uliopita pamoja na ubora wa Yanga na wao wamejiandaa kuhakikisha wanapata matokeo.
”Hii ni mechi mpya na kutakuwa na mbinu tofauti, tuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza mechi kama hizi hivyo tumewaandaa vizuri kuhakikisha tunakuwa bora,” amesema Matola na kuongeza;
“Tumejiandaa ki dabi kuhakikisha kesho tunapata matokeo, hatuna presha yoyote kwasababu ni mchezo ambao sio wa kwetu kucheza wanaamini katika jitihada na mbinu.”
Matola alisema wamefanyia kazi safu yao ya ushambuliaji kuhakikisha wanazitumia nafasi wanazozitengeneza ili kuweza kupata matokeo huku akikiri kuwa iwe mvua liwe jua wamejiandaa kwenye hali zote.
Simba watashuka Dimba la Mkapa wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza wakiwa nyumbani kwa kichapo cha mabao 5-1.