AIC Nira Gospel Choir, Lemi George wazidi kupaa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwimbaji wa gospo kutoka jijini Mwanza, Lemi George na kwaya ya AIC Nira, wamefanikiwa kujizolea mashabiki wapya kupitia wimbo wao mpya, Msalabani.

Akizungumza na mtanzania.co.tz leo, Lemi, alisema anamshukuru Mungu kwa mapokezi makubwa ya video ya wimbo huo ambao umefanya vizuri katika msimu wa sikukuu ya Pasaka.

“Huu ni upendo mkubwa ambao mashabiki wa Injili wametuonyesha mimi na AIC Nira Gospel Choir ya hapa Nyakato Mwanza, video tayari ipo kwenye chaneli yetu yao ya YouTube na bado tunaomba sapoti ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi pia hivi karibuni tumeachia wimbo Mungu wa Rehema ambao tayari upo mtandaoni,” amesema Lemi.

Related Posts