DORIS MOLLEL, ORYX GAS KUTOA NISHATI SAFI KWA WAUGUZI 1000 – MWANAHARAKATI MZALENDO

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation wamekabidhi mitungi
ya gesi ya kupikia ya Oryx 50 kwa wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala jijini Dar es Salaam kati ya mitungi  1000  inayotarajiwa
kukabidhiwa kwa wauguzi na madaktari katika mikoa 10 nchini .

Akizungumza
wakati wakisaini makubaliano ya ushirikiano yaliyofanyika katika
hospitali ya rufaa ya Mwananyama, Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx
Araman Benoite amesema makubaliano walioingia baina ys kampuni hiyo na
taasisi ya Doris Mollel ni kusaidia kuongeza matumizi ya nishati safi ya
kupikia kwa watanzania.

Aidha
amesema katika kampeni hiyo ya kuwezesha watanzania kuingia katika
matumizi ya nishati safi ya kupikia, mpaka sasa tayari wameshatoa
mitungi kwa wananchi zaidi ya elfu 32 ili kusaidia lengo la kufikia
asilimia 80 ya watumiaji wa nishati safi.

Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia inasaidia kuondoa hatari za kiafya
kwa watumiaji wa kuni na mkaa kama nishati ya kupikia lakini pia hatari
za kimazingira na ustawi wa jamii.

“Takribani watu 33,000 wanapoteza maisha nchini Tanzania kwa maradhi yanayotokana
na kuvuta moshi unaotokana na mkaa au kuni hiyo ndio sababu ya Oryx gas
kuja na suluhisho la kuwahamasisha wananchi kutumia gesi kwa matumizi ya
kupikia”, amesema Benoite

Ameeleza
kuwa matumizi ya gesi yanaepusha wamama na watoto kuumika kubeba kuni
hivyo kuepuka kujeuriwa na wanyama wakali wakiwa katika harakati za
kutafuta kuni pia kuimarisha maisha ya wanawake na kuwalinda dhidi ya
vitendo vya udhalilishaji.

“Kuanzia
mwezi wa saba mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kuunga mkono
utekelezaji wa mkakati wa serikali uliopewa nguvu na Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania , Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo kwamba ifikapo
mwaka 2033 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya
kupikia”, ameeleza.

Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel
amesema katika makubaliano waliosaini na oryxy watawafikia waguzi elfu
moja ambapo watawapa mitungi na majiko ya gesi kama mabalozi kwa kina
mama waweze kutumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni programu ya miaka
miwili.

Amesema
mitungi hiyo itakwenda kwa wauguzi walioko maeneo magumu ambapo
watakuwa wanawatembelea kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuweza
kuwafikia wafanyakazi ambao ni wauguzi wanaofanya kazi kubwa ya kuokoa
maisha hususani ya mama na mtoto.

Wakati
huo huo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala  Dk.Zavery
Benela ameeleza kwamba hospitali hiyo  inakabiliwa na ongezeko la
wagonjwa wa mifumo ya hewa.

Amefafanua
kati ya wagonjwa wa nje 500 wanaofika kuonwa na madaktari bingwa
asilimia 30 ya wagonjwa hao ni wa matatizo ya mfumo wa hali ya hewa
unaosababishwa na hali ya hewa pamoja na mazingira ya kuandaa chakula
kutokna na kuni na mkaa.

Aidha Dokta Benela amesema magonjwa ya mfumo wa hali wa hewa  yamekuwa changamoto hasa kwa watu wazima na watoto.

 

Mkurugenzi
wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya
Doris Mollel , Doris Mollel wakionesha mkataba waliosaini  kwaajili ya
kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka
mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa
kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni
na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Oryx Gas kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Oryx Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel (katikati) akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubalinao na Kampuni ya Oryx Gas kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam  Dk.Zavery Benela akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini na Taasisi ya Doris Mollel kushirikiana kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10 nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakionesha mkataba waliosaini  kwaajili ya kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel wakimkabidhi mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx mmoja wa wauguzi katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini makubalino kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

Mkurugenzi wa Kampuni ya gesi ya oryx Araman Benoite  akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Oryx kwa wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala katika hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.



Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala wakifuatilia hafla ya utiaji saini kati ya kampuni ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kuwezesha nishati safi ya kupikia kwa wauguzi na madaktari 1000 kutoka mikoa 10  nchini watakabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx Gas lengo likiwa kuliwezesha kundi hilo la sekta ya afya kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2024.

 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Related Posts