Gamondi, Benchikha wakutana na sapraizi Kwa Mkapa

Unaweza kusema ni kama makocha wa timu zote mbili, Miguel Gamondi wa Yanga na Abdelhak Benchikha wa Simba wamekutana na sapraizi, baada ya kulazimika kufanya mabadiliko ya mapema zaidi.

Kwa kawaida, mabadiliko ya wachezaji kwenye mechi hufanyika kiufundi, lakini jana makocha hao walilazimika kuyafanya mapema bila ya kutarajiwa.

Alianza Gamondi kufanya mabadiliko ya kumtoa Joyce Lomalisa dakika ya 6 ya mchezo huo, baada ya beki huyo wa kushoto kuonekana kuugulia nyama za paja, nafasi yake ikachukuliwa na Nickson Kibabage.

Dakika 5 baadaye kwa maana ya ilipofika 11 tangu kuanza kwa mchezo huo, Benchikha naye alilazimika kumtoa Henock Inonga na kuingia Hussein Kazi.

Inonga alionekana mapema tu akichechemea tangu kuanza kwa mchezo huo ikionekana akisumbuliwa na misuli, lakini baadaye alipokuja kugongana na Clement Mzize, ikawa ndiyo mwisho wa kuendelea. Akatolewa.

Related Posts