JKT yaichapa Geita Queens 9-0, Stumai akiweka matano WPL

LEO saa 4:00 asubuhi katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo ilipigwa mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), JKT Queens ikiwa nyumbani na kuondoka na ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Geita Queens.

Mabao yalifungwa na Stumai Abdallah aliyeweka kambani matano, Winifrida Gerald, Alia Fikirini, Donisia Minja na Lydia Maximilian waliofunga moja kila mmoja.

Kwa matokeo hayo yanamfanya Stumai aongoze kwenye vita ya ufungaji kwa kufikisha mabao 16 nyuma ya Asha Mnunka wa Simba Queens mwenye nayo 13 na Asha Djafar aliyeweka nyavuni manane.

Hadi sasa Simba Queens inaendelea kupigania malengo ya kubeba ubingwa kwa kutopoteza michezo 11 ya ligi na kuipa wakati mgumu wa kutetea taji inaloshikilia  JKT.

Zikiwa zimesalia mechi saba Simba Queens bado inaongoza kwenye msimamo na pointi 31, JKT pointi 25 na Yanga yenye pointi 21 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Wakati Simba Queens na JKT zikipambania nafasi za juu, Alliance Girls ambayo ilikuwa mkiani imesogea hadi nafasi ya tisa na kufikisha pointi saba baada ya kutoka sare ya maba 2-2 na Geita Queens na kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bunda Queens, jana.

Baada ya mechi hizo Alhamisi ijayo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, utashuhudia dabi ya kinadada Simba Queens na Yanga Princess, JKT Queens dhidi ya wanajeshi wenzao Amani Queens (Mashujaa Queens), Fountain Gate Princess na Alliance Girls, Bunda Wueens na Baobab Queens huku Geita ikiikabili Ceasiaa Queens.  

Related Posts