Mtangazaji wa Clouds Gardner afariki, mastaa wamlilia

Dar es Salaam. Kufuatia taarifa ya kicho cha mtangazaji maarufu wa Kampuni ya Clouds Media, Gardner G Habash, watu mbalimbali wakiwemo wasanii na watu wanaomfahamu wametuma salamu za rambirambi kwa familia yake.

Gardner amefariki dunia leo April 20,2024  saa 11 alfajiri  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakati akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyomsumbua.

Taarifa ya kifo cha Gardner imethibitishwa na Msemaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Emilian Mallya.

 “Ni kweli kwa taarifa za awali amefariki dunia, lakini nitatoa taarifa zaidi baadaye,” amesema Mallya.

Aliyewahi kuwa mfanyakazi mwenzake, Zamaradi Mketema kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika, “Aaah Gardner jamani!!! Inalillahi waina ilaihi rajiun!!! Mungu akupumzishe kwa amani kaka, Dah!!! Gardner, pumzika kwa amani kaka!!! Kazi ya Mungu haina makossa.”
Naye msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu kupitia Instagram amendika,“Daaaah aiseee😭😭😭😭💔💔💔💔 Pumzika Brother Gardner.”

Mwingine ni muingizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere ambaye naye kupitia mtandao huo wa Instagram ameandika, “Mstafuuuuu. Hapa duniani tunapita na barabara tunayopita ni wote tutapita hiyo hiyo, bahati nzuri njia tunayopita kila mmoja ana muda wake wa kupita, lakini atapita tu.”

“Katika ukurasa huo ameendelea kuandika kuwa, “Maskini atapita, tajiri atapita, mh atapita, chizi atapita lakini tumepishana saa tu.
Steve ameandika kuwa, ” Mungu kaweka siri kubwa kwenye kifo na ndio maana mpaka leo tumekuwa watu wa kusema Mungu nisaidie kifo chema..

“Kaka lala, tutaonana baadaye. Ni ngumu kuamini, lakini kwa mapenzi ya Mungu kila jambo linawezekana…..”amehitimisha andiko lake
Msanii Dulla Makabila kupitia Instagram yake aliandika “Rest in Peace brother Gardner 😭😭😭😭😭😭😭.Mungu aitie nguvu familia ndugu jamaa na marafiki kwenye kipindi hiki kigumu.

Naye mtoto wa marehemu Kingunge Ngombale Mwiru, Kijekitile Ngombare maarufu Kinje kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika,”Rest in peace mdogo wangu,  juzi nimekuja kukuona nikakuambia nitakuja kukuona tena, daah pumzika kwa amani mdogo wangu.”

Gardner alijipatia umaarufu kupitia kipindi cha Jahazi wakati huo akishirikiana na Ephraim Kibonde ambaye sasa ni marehemu na Paul James maarufu kama PJ ambapo kipinci hicho kilikuwa kikirushwa hewani kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 12 jioni.

Related Posts