CAG atilia shaka uadilifu wa Viongozi wa Manispaa ya Temeke ,Njombe.

*Ni utoaji wa mikopo wa fedha zaidi ya kilichoombwa

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na Njombe zilitoa mikopo zaidi ya kilichoombwa hali hiyo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CPA Charles Kichere ametia shaka juu ya utoaji mikopo zaidi kilichoombwa.

Halmashauri ya Temeke ilitoa fedha kwa vikundi 12 kutoa zaidi ya sh. Milioni 64 huku Halmashauri ya Njombe ikitoa sh.milioni 20 kwa kikundi kimoja.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya imebaini kutoa mikopo zaidi ya kiasi kilichoombwa kunatia shaka juu ya uadilifu wa viongozi wa halmashauri husika.

Katika ripoti hiyo ya Halmashauri kutoa fedha zaidi kile kilichokuwa kinahitajika amependekeza halmashauri husika zihakikishe masuala yote ya kisheria yanashughulikiwa kikamilifu kabla ya fedha kutolewa.

CAG kwa mujibu wa ripoti hiyo kufuatwa taratibu hizo itasaidia kupunguza migogoro inayoweza kutokea, kulinda maslahi ya pande zote mbili na kuweka mfumo thabiti wa kisheria.

Pamoja na yote CAG alibainisha pia kutoa mikopo kulingana na maandiko ya Miradi ya kikundi yaliyowasilishwa, na ikihitajika kutoa zaidi ya kiasi cha mkopo ulioombwa, vikundi vitapaswa kutoa sababu zilizothibitishwa.

Mapitio ya utendaji wa Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Mikopo kwa Asilimia Kumi (TPLMIS) Upungufu wa TPLMIS Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Mikopo kwa Asilimia Kumi ulianzishwa
ili kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utoaji wa mikopo, usimamizi na urejeshaji wa mikopo iliyotolewa kwa Wanawake, Vijana na vikundi vya watu wenye ulemavu.

Mfumo huo ulianzishwa mahususi ili kupunguza msongamano wa wananchi katika ofisi ya halmashauri, kwani unaruhusu mtu yeyote kujiandikisha kutoka mahali popote.

Kufuata kwa mifumo unazuia kurudiwa kwa majina ya vikundi kwa sababu mfumo huo ulikusudiwa kusajili jina la kikundi mara moja tu. Mfumo unasaidia katika Kuweka kumbukumbu za vikundi kwa kuwa kitabu cha usajili tayari kipo kwenye mfumo na kuwazuia watu binafsi kuchukua mikopo mingi bila kurejesha mikopo iliyotolewa awali kwa vile mfumo unatumia namba za NIDA ambazo hukubali kuingizwa kwenye mfumo.

Related Posts