NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, KIGOMA
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Deogratius Ndejembi amewahakikishia Majaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na
wadau wengine kuwa, Serikali inayachukulia kwa uzito mkubwa maoni yao kuhusu
kuboresha baadhi ya vifungu vya sheria ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia,
kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Mhe.
Ndejembi ameyasema hayo wakati wa kufunga kikao kazi kati ya Waheshimiwa Majaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kati ya Magharibi,
Kamishna wa Kazi, Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi na Tume ya
Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Aprili 20, 2024 Mkoani Kigoma.
“Tayari
maoni mliyotoa ya kuboresha kifungu cha 39 (2) cha Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi [Sura 263] kilichoweka ukomo wa muda wa kuwasilisha madai bila
kutoa wigo wa kupokea madai hayo iwapo kuna sababu za msingi za kucheleweshwa
kwake, tumeshayafanyia kazi na maboresho hayo kuwa sehemu ya muswada wa
marekebisho ya Sheria za Hifadhi ya Jamii uliosomwa Bungeni kwa mara ya kwanza
tarehe 15 Februari 2024.” Amefafanua.
Aidha
Mhe. Ndejembi amesema, WCF kwa kushirikiana na Kurugenzi ya Hifadhi ya Jamii
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), wanaendelea na
uchambuzi wa maboresho ya sheria ya fidia kwa wafanyakazi ambayo yalitolewa na
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi.
Awali
akifungua kikao hicho Aprili 19, 2024, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa
Ibrahim Hamisi Juma, amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema
lengo la vyombo vyote vya dola ni ustawi wa wananchi, WCF kama chombo cha
serikali inagusa ustawi wa wananchi.
“WCF
ni Mfuko unaogusa ustawi wa wananchi, kwasababu unaweza kuwa unamtegemea mama,
kaka, bahati mbaya akapata ajali akafariki, hapa ustawi wa familia unaweza kutoweka,
kama hakuna Mfuko unaoweza kubeba hilo jukumu, kwa hivyo huu Mfuko ni muhimu
mno mno.” Amebainisha Mhe. Profesa Juma.
Aidha
Mhe. Profesa Juma amehimiza umakini na uadilifu katika utekelezaji wa sheria
hiyo ya Fidia kwa Wafanyakazi.
“Ukosefu
wa umakini, udanganyifu vyote vimechangia kuua mifuko ambayo ilikuwa na malengo
mazuri sana. Tusipokuwa waangalifu, mfuko huu wa WCF vile vile unaweza
kukumbana na tatizo hili. Tukielewa vizuri mantiki ya kuanzishwa mfuko huu
tutaufanya uwe endelevu na himilivu,” amesema.
Aidha
Mhe. Jaji Mkuu ameipongeza WCF kwa kupiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA
katika utekelezaji wa majukumu yake na kukumbusha umuhimu wa mifumo ya taasisi
za umma kusomana ili kurahisisha utoaji wa huduma.
“Ifike
mahala mfanyakazi anapowasilisha madai yake WCF, mfumo mzima uwe unaelewa
kwamba mfanyakazi fulani amepata ajali kazini au amefariki. Mifumo ya serikali
ikiweza kutambuana pia itasaidia sana kuziba mianya ya udanganyifu.”
Alisisitiza.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw.
Emmanuel Humba, amesema Bodi na Menejiment ya WCF wataendelea kushirikiana na
Mahakama
Akizungumzia
kuhusu nia ya kikao kazi hicho, Bw. Humba alibainisha kuwa pamoja na kwamba
jukumu la kulipa fidia limekasimiwa kwenye Mfuko, Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi imeweka utaratibu na vyombo vya kushughulikia madai ya wanufaika
pale wanapokuwa hawajaridhika na fidia iliyolipwa au maamuzi ya Mfuko
yanayokinzana na matarajio yao.
“Kutokana
na hitaji hili muhimu la kisheria, Bodi ya Wadhamini ya WCF, Menejimenti ya
Mfuko pamoja na Watendaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi waliona kuna hitaji
la kufanya vikao kazi kwa lengo la kubadilisha uzoefu, kujenga uelewa wa pamoja
na kubainisha maeneo ya sheria yanayohitaji maboresho kwa lengo la kuongeza
ufanisi katika kutekeleza Sheria hiyo.” Alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John
Mduma ameeleza kuwa ushirikiano baina ya Mfuko na Mahakama ni muhimu kwa vile
kuna maeneo mengi ambayo Mfuko unakutana na Mahakama katika utekelezaji wa
majukumu yake.
“Sisi
kama WCF shughuli zetu hazikamiliki bila ya uwepo wa shughuli za Mahakama. Kwa
mfano katika kushughulikia masuala yanayohusu mirathi, Mfuko hutegemea maamuzi
ya Mahakama.” Alisema Dkt. Mduma
Alisema
kuwa Mfuko umefanya vikao kazi vitano ambavyo vimefanyika baina ya Mahakama,
WCF na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Deogratius Ndejembi (kulia), akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, baada ya kufunga kikao kazi kati ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kati ya Magharibi, Kamishna wa
Kazi, Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na
Uamuzi (CMA) Aprili 20, 2024 Mkoani Kigoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, WCF, Bw. Emmanuel Humba.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Deogratius Ndejembi, akifunga kikao kazi kati ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kati ya Magharibi, Kamishna wa
Kazi, Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
(CMA) Aprili 20, 2024 Mkoani Kigoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe.
Deogratius Ndejembi, akifunga kikao kazi kati ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kati ya Magharibi, Kamishna wa
Kazi, Menejimenti ya Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
(CMA) Aprili 20, 2024 Mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, WCF, Bw. Emmanuel Humba, akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akizungumza mwanzo mwa kikao hicho.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, akielezea historia ya viao kazi baina ya Mfuko na Mahakama.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho
Mhe. Ndejembi, akizunguzma jambo na Dkt. Mduma.
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho
Mhe.
Aziza Iddi Swedi, Jaji Mwenye dhamana ya Divisheni ya Kazi Mahakama Kuu,
Zanzibar, akieleza uzoefu wa sharia inayosimamia masuala ya fidia kwa wafanyakazi
huko Zanzibar.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho Mhe. Jaji Abdi Kagomba, akichangia mjadala kuhusu sheria ya fidia kwa wafanyakazi.