Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni
mpya ya akiba inayofahamika kama “Shinda Mechi Zako Kinamna Yako”
mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa,
wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi.
Ujio wa kampeni hiyo
inayoambatana na zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za gari mbili aina ya BMW x1,
unalenga kuimarisha ustawi wa kifedha miongoni mwa wateja hao sambamba na
kuunga mkono jitihada za serikali katika kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia utoaji
wa huduma rasmi za kifedha na kukuza
uchumi jumuishi.
Akizungumzia kampeni
hiyo kwenye hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo,
wateja na waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC Bw David
Raymond alisema inahusisha wateja wa rika zote wanaohudumiwa na benki kupitia
huduma zake mbalimbali.
“Tunaposema shinda
mechi zako kupitia kampeni hii tunalenga kuitumia falsafa ya mchezo wa soka
ambao Benki ya NBC ndio wadhamini wakuu wa ligi tatu muhimu hapa nchini ikiwemo
Ligi ya Soka ya Tanzania Bara yaani NBC Premier League. Tunapoingiza falsafa hiyo
kwenye maisha ni wazi tunatambua wateja wetu wana ndoto, malengo na maazimio
mbalimbali katika kufanikisha maendeleo yao hususani kiuchumi ikiwemo ujenzi,
kukuza biashara zao, kusomesha watoto na mengine mengi.
‘’Hivyo basi tukiwa
kama benki tunayowahudumia tunaona wazi kuwa tunao wajibu wa kuwasaidia wateja
hawa kufanikisha malengo hayo na hiyo ndio maana ya wao kushinda mechi zao.
Kupitia mkakati huu tunahusisha agenda ya msingi kabisa ambayo kwanza ni kutoa
elimu na kuwashawishi watumie huduma zetu rasmi za kibenki zinazogusa rika na
makundi yote ya kijamii kuanzia watoto hadi wazee’’ alifafanua.
Alitaja huduma
zinazohusishwa na kampeni hiyo kuwa ni pamoja na akaunti ya Chanua ambayo ni
mahususi kwa watoto, Akaunti ya Malengo, Akaunti ya Johari mahususi kwa
wanawake, Akaunti ya Mwalimu, Akaunti ya Mshahara, Akauti ya Wajasiriamali,
Akaunti ya Wanafunzi, Akaunti ya Kua Nasi, Akaunti ya Vikundi, Akaunti Binafsi
na Akaunti ya Biashara.
Akizungumzia zawadi
mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni hiyo, Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki
ya NBC, Bi Dorothea Mabonye alisema kampeni hiyo ya mwaka mmoja inahusisha
zawadi za kila mwezi na mwisho wa mwaka ikiwemo zawadi kuu ya gari aina BMW X1
zitakazotolewa kwa washindi wawili, fedha taslimu, zawadi ya safari ya
mapumziko nchini Singapore, simu za mikononi, ‘laptops’, friji, tablets za
watoto pamoja na majiko ya kisasa ya kupikia.
“Tunawahimiza tu
wateja wetu wapya na waliopo wajitokeze kwa wingi wafungue akaunti na waweke
akiba zaidi ili waweze kuingia kwenye droo zitakazowawezesha kushinda zawadi
hizi,’’ alibainisha.
Mkuu wa Kitengo cha
Masoko wa NBC Bw David Raymond (wa pili kushoto) akiwaonesha wadau mbalimbali
wa benki hiyo wakiwemo waandishi wa habari gari aina BMW x1 itakayotolewa kwa
mshindi wa kampeni ya akiba “Shinda Mechi Zako Kinamna Yako” ya benki
hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi,
waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni
hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.
Meneja
Masoko wa NBC Alina Kimaryo (wa tano kushoto) sambamba
na Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye (wan ne kushoto) wakiwaonesha wadau mbalimbali
wa benki hiyo wakiwemo waandishi wa habari gari aina BMW x1 itakayotolewa kwa
mshindi wa kampeni ya akiba “Shinda Mechi Zako Kinamna Yako” ya benki
hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi,
waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni
hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.
Mkuu wa Kitengo cha
Masoko wa NBC Bw David Raymond (Kulia) na Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya
NBC, Bi Dorothea Mabonye (kushoto) wakitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kampeni ya akiba “Shinda Mechi
Zako Kinamna Yako” ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina
mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na
wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo,
wateja na waandishi wa Habari.
Meneja Masoko wa NBC
Alina Kimaryo (kushoto) na Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea
Mabonye (wa pili kulia) wakitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kampeni ya akiba “Shinda Mechi
Zako Kinamna Yako” ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina
mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na
wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo,
wateja na waandishi wa Habari.
Baadhi ya wafanyakazi
wa Benki ya NBC wakifuatilia hafla ya uzinduzi kampeni ya akiba “Shinda
Mechi Zako Kinamna Yako” ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina
mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na
wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo,
wateja na waandishi wa Habari.
Akizungumzia kampeni
hiyo mmoja wa mabalozi wa benki ya NBC, Nasry Ramadhani ‘Ujugu’ (Katikati)
ambae ni mjasiriamali aliwekeza kwenye biashara ya kuonesha burudani ya mpira
kupitia TV kwenye mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam aliwasihi wajasiriamali
mbalimbali wakiwemo vijana kutumia vema fursa hiyo iliyotolewa na benki ya NBC
kupitia kampeni hiyo ili waweze kunufaika kupitia faida mbalimbali zitokanazo
na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.
Wafanyakazi wa benki
ya NBC, mabalozi wa benki hiyo pamoja na waandishi wa habari wakijipongeza wakati
wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya akiba “Shinda Mechi Zako Kinamna
Yako” ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo
wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya
uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na
waandishi wa Habari.