Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa na ngurumo kwa mikoa 26 ya Tanzania Bara na visiwa vya Unguja na Pemba kuanzia leo Aprili 22, 2024.
Mikoa ambayo inapata mvua leo Aprili 22, 2024 kwa mujibu wa TMA ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Dodoma, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe. Pia visiwa vya Unguja na Pemba.
“Angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya Mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba,” imeandikwa kwenye taarifa ya TMA ya matarajio ya hali mbaya ya hewa ya siku tano kuanzia jana Aprili 21, 2024.
Kwa siku ya leo angalizo la uwepo wa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa kufikia mita mbili, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani.
TMA kupitia taarifa imesema Aprili 23, angalizo la mvua kubwa linatolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba.
“Angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa kufikia mita mbili, limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoo ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba),” imeeleza taarifa hiyo.
Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani
Angalizo la mvua kubwa limetolewa katika maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba.
Pia, angalizo la upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa Pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.
Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani
Agalizo la mvua kubwa limetolewa katika Mkoa wa Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.
Kiwango cha athari ambayo imeelezwa na TMA kutokana na mvua hizo ni wastani.