Toshiba yapata kibali cha kuzalisha vifaa umeme kukarabati kiwanda cha nishati ya jotoardhi Kenya.

· Mitambo na jenereta zenye ufanisi wa hali ya juu za Toshiba imeboresha uzalishaji wa umeme kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miundo ya kawaida.

NAIROBI. Kampuni ya Toshiba Energy Systems & Solutions Corporation (Toshiba ESS) imefanikiwa kupata kibali kutoka kwa SEPCOIII Electric Power Construction Co., Ltd. kwa ajili ya mitambo ya mvuke na jenereta na ukarabati wa mitambo ya nishati ya jotoardhi ya Unit 1 hadi 3 kwenye mtambo wa zamani wa 45MW Olkaria I wa nishati ya mvuke nchini Kenya. Mitambo ya mvuke na jenereta itasafirishwa mpaka eneo husika kufikia Desemba 2025.

Kiwanda cha kuzalisha umeme kwa jotoardhi cha Olkaria I ndicho mtambo kongwe zaidi wa kuzalisha umeme wa mvuke nchini Kenya na kimekuwa kikiendeshwa kibiashara na Kenya Electricity Generating Company PLC (ikijulikana kama “KenGen”) tangu 1981.

Sehemu ya 1 hadi 3 ya mtambo huo inahitaji kurekebishwa kutokana na kuzeeka, na mitambo na jenereta za mvuke za Toshiba ESS zimechaguliwa kwa ukarabati. Hii itaongeza pato la umeme la Units 1 hadi 3 kutoka Megawati 15 za sasa (MW) mpaka MW 21 kwa kila mojawapo, na kuiwezesha kufikia uzalishaji wa juu kwa kutumia mvuke kidogo. Hoja hizi zilitathminiwa kwa kina na KenGen na kupelekea kupitishwa kwa mkataba.

Ukuaji wa uchumi wa Kenya unachochea mahitaji ya nishati. Serikali imejibu kwa mpango wa kina wa maendeleo, Dira ya 2030, ambayo kwa sasa inajumuisha utoaji wa kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme wa Kenya kutoka katika vyanzo mbadala na kupitia mabadiliko ya mpaka asilimia 100 ya nishati ya kijani ifikapo 2030. Mitambo mingi mipya ya nishati ya jotoardhi imepangwa kuingia katika Uwezo wa mvuke wa 9GW katika eneo la Bonde la Ufa la Kenya.

Toshiba ESS na KenGen walihitimisha mkataba wa maelewano (MOU) wa kutarajia ushirikiano katika huduma za Uendeshaji na Matengenezo kupitia ushirikiano wa ujuzi na mitandao ya KenGen na Toshiba ESS mwaka 2022. Wanalenga kutoa huduma za uendeshaji na matengenezo kwa mitambo ya nishati ya jotoardhi kwa nchi zinazoendelea zikiwemo nchi za Afrika Mashariki nje ya Kenya.

Toshiba ESS ina rekodi kadhaa za ufanishi wenye mafanikio zinazotoa mifumo ya uzalishaji wa nishati ya jotoardhi nchini Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kwa kuongezea, Toshiba ESS imechangia katika kukuza uzalishaji wa nishati ya jotoardhi kwa kutia saini makubaliano ya biashara ya mitambo ya umeme wa mvuke na washirika kadhaa katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Shinya Fujitsuka, Mkurugenzi na Makamu wa Rais wa Kitengo cha Mifumo ya Umeme wa Toshiba ESS, alisema, “Nina furaha kwamba tunaweza kuchangia uthabiti wa nishati nchini Kenya kwa kutoa vifaa na huduma zetu. Toshiba ESS itaendelea kutoa bidhaa na suluhisho bora zaidi za kukidhi mahitaji ya wateja kupitia aina tofuati ya mitambo midogo hadi mikubwa ya mvuke ya jotoardhi na jenereta zenye uzalishaji wa nishati kuanzia MW 1 hadi MW 200.

 Tukilenga kuwezesha nishati safi zaidi ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuwa na jamii endelevu, tutachangia katika kukamilisha ndoto ya kuwa na jamii isiyo na kaboni kwa kutoa huduma za mitambo ya nishati ya jotoardhi nchini Japani na nje ya nchi”.

 

Related Posts