Vijiji 52 Mvomero kunufaika na mradi wa LTIP

Vijiji takribani 52 katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro vitanufaika na Mradi waUboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) kwa kuandaliwa mipango ya matumizi yaardhi ya vijiji.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bi. Judith Nguli wakati wa kujadiliutekelezaji wa Mradi huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mvomero, tarehe 22 Aprili 2024 Mkoani Morogoro.

Alisema kupitia mradi huu lengo ni kuandaa jumla ya Mipango Shirikishi ya Matumizi yaArdhi ya Vijiji 52 katika Wilaya ya Mvomero ambapo hadi kufikia sasa tayari mipango 48 imekwishaandaliwa.

‘‘Tarafa nne zilizopo Mvomero zitakazonufaika na mradi huu ni Tarafa ya Mgeta – vijiji 19, Tarafa ya Mvomero – vijiji 11, Tarafa ya Mlali – vijiji 11 na Tarafa ya Turiani – vijiji 11ambavyo kwa pamoja vitakuwa na jumla ya mipango ya matumizi ya ardhi 52’’ alisemaNguli.

Msimamizi wa Mradi katika Wilaya ya Mvomero Bw. Sambalu Simon amesema kuwa lengola kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji ni kuimarisha milki za ardhi na matumiziyake, kugawa ardhi na kuboresha matumizi na hifadhi ya ardhi kulingana na mapendekezo nauwezo wa Kijiji, kubaini na kutenga maeneo ya umma pamoja na kuimarisha utunzaji wamazingira kupitia sheria ndogo zinazotungwa kusimamia mpango.

Nae Bi.Sofia Lucas mkazi katika Wilaya ya Mvomero alimshukuru Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka mradi huo Wilayani kwao, kwakuwa mradi umewekeza sana katika kutoa elimu kwa jamii hususani makundi maalumu kamaushiriki wa wanawake katika kumiliki ardhi ili kuwakomboa kiuchumi.

Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi umeweka nguvu kubwa katika kutoa elimu kwa wananchikuanzia ngazi ya Kitaifa, Wilaya, Mtaa/Kijiji mpaka Kitongoji ikiwa ni pamoja na kuzingatiahaki za makundi mbalimbali yakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi, wanawake, vijana, wenye ulemavu sambamba na utoaji wa elimu ya usawa wa jinsia katika umiliki wa Ardhi ilikuhakikisha usalama kwa kila kipande cha ardhi kwa Mtanzania.

Related Posts