BUNGE LAPITISHA BAJETI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti ya Ofisi
ya Makamu wa Rais kiasi cha shilingi bilioni 62.7 kwa mwaka wa fedha
2024/2025 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 23, 2024.

Hotuba ya bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ilichangiwa
na wabunge mbalimbali ambao baadhi yao wamepongeza jitihada za
Serikali za kutatua hoja za Muungano na namna inavyoshughulikia
hifadhi ya mazingira.

Awali akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizojitokeza wakati wa
majadiliano, Waziri Dkt. Selemani Jafo amelihakikishia Bunge kuwa hoja
nne zipo katika hatua za utatuzi.

Amesema faida za Muungano ni nyingi zikiwemo mahusiano mazuri kati
ya wananchi wa pande zote mbili na hivyo kufanya biashara pamoja na
kujenga uchumi.

Kwa upande wa mazingira Dkt. Jafo amesema kutokana na biashara ya
kaboni kushika kasi Serikali imeamua kujenga uwezo kwa wataalamu wa
mazingira katika Serikali za Mitaa ili wananchi waweze kushiriki
kikamilifu.

Hata hivyo, amesema athari za mabadiliko ya tabianchi ni kubwa na
kutokana na hali hiyo Serikali inaendeleza jitihada za kuhakikisha
mazingira yanahifadhiwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
MazingiraO Mhe. Khamis Hamza Khamis akichangia hoja amesema elimu
ya Muungano itaendelea kutolewa ili wananchi wapate uwelewa Zaidi na
kuuenzi Muungano.

Amesema elimu ya Muungano inatolewa wakati wowote kupitia
makongomano mbalimbali huku akiongeza kuwa kutokana na umuhimu
huo Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa kitabu kitakachoelimisha
wananchio kuhusu Muuungano wakati wote.

Related Posts