Na Mwandishi Wetu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) Bi Beng’i Issa amesema kuwa katika miaka sita ya Rais Dkt.SamiaSuluhu Hassan kimekuwa na mapinduzi katika uwekeaji nchini kwa wazawa.
Beng’i ameyasema hayo wakati wa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kongamano la nne la Ushiriki wa Watanzania kwenye uchumi na Uwekezaji (Local Content) litakalofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 mwezi huu
Amesema kuwa Kongamano hilo hufanyika kila baada ya miaka miwili ikiwa ni pamoja kuangalia tathimini ya miaka miwili iliyopita na kuweka dira ya miaka miwili katika uwekezaji kwa wazawa.
Amesema , mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Mashaka Biteko.
Amesema kuwa Kongamano hilo litaweka picha ya kuweza kukua Kwa uwekezaji wa wazawa.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo picha) kuhusu kongamano la nne la Ushiriki wa Watanzania kwenye uchumi na Uwekezaji (Local Content) litakalofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 28 mwezi huu ambalo hufanyika Kila baada ya miaka miwili , mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Dkt Dotto Mashaka Biteko .