Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akutana na mkuu wa idara ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa Bw. Jean Pierre Lacroix ofisini kwa Mkuu wa Majeshi, Upanga, Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo yao, Bw. Jean Pierre Lacroix amelipongeza JWTZ na kusema Umoja wa Mataifa unaridhishwa na weledi na utendaji kazi wa JWTZ katika operesheni za ulinzi wa amani sehemu mbalimbali duniani.

Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kuliamini JWTZ na kuwahakikishia kuwa JWTZ liko imara na litaendelea kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani duniani wakati wowote litakapohitajika.

Related Posts