MKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Mulembo, aliyempinga Mbunge wa Kisesa, Lwaga Mpina. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Hivi karibuni, Mpina alikaririwa akitaka Serikali iunde Tume kuchunguza kifo cha Rais John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 mwaka 2021 na nafasi yake kuchukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mjadala kuhusu uchunguzi juu ya kifo cha Magufuli, umeibuka tena hivi karibuni baada ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo kuibua mjadala tata namna walivyovutana na vigogo wenzake kuhusu kutangaza kifo cha Rais Magufuli, maziko yake na namna ya kurithisha kiti chake kwa Makamu wake, Dk. Samia.
Andiko la Shibuda ambaye amepata kuwa Mbunge wa Maswa Mashariki kupitia Chadema na Mwenyekiti wa Wazazi CCM, ilisomeka hivi;
Shibuda anaanza kwa kusema, Salamu zangu kwako ndugu Bulembo. Natumaini hujambo na unaendelea salama na ujenzi wa ustawi na maendeleo mema daima kwa, yako famili na kwa jamii na letu taifa.
Ndugu Bulembo, nimeona andiko lako la wito wenye utashi wa matakwa ya hitaji la hatua za nidhamu dhidi ya ndugu Mpina. Vivyo ukatia umwambatano wa yako hoja kwa Comrade Kinana.
Kwangu mimi ndugu Mpina ni mtumishi wa kutumikia imani, malengo na shabaha za CCM Party Destiny kwa jamii na kwa letu hili taifa la Tanzania. Mpina anawajibika kwa Katiba ya CCM na kwa Katiba ya nchi yetu ya taifa hili la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ambayo in principle na kwa kanuni za Bunge la Jamhuri ya Muungani la Tanzania.
Kwangu mimi nahitaji mhali wa maslahi sahihi ya hatma ya CCM kwa maslahi sahihi ya CCM kwa jamii na kwa taifa hili.
Ndugu Bulembo, kumbuka vilevile pana wajibu wenye maslahi sahihi kwa masuala chanya ya wana jamii wa taifa letu. Hayati Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alihusia hekima inenayo—-Tujisahihishe.
Ndugu yangu Bulembo, shilingi ina pande mbili. Wewe umenena yako ya upande mmoja wa shilingi, Je, kulikoni ndani ya upande wa pili wa shilingi? Wito wako adhimu umenifikirisha.
Ndugu, Bulembo, pana tafakari makini ndani ya andiko lako na lina deni linalohitaji malipo ya wianisho la mawazo ya fikra sahihi za pande mbili za shilingi.
Ndugu Bulembo, aulizae ataka kujua. Adui ujinga haondolewi kwa viboko bali kwa elimu. Punda hupigwa sana mijeledi, je amebadirika na kuwa Profesa ? La hasha.
Ndugu Bulembo, vitendawili hasi havitenguliwi kwa bakora bali hukunjuliwa na turufu yenye mapiku sahihi ya msemaji wa imani njema kwa kiu ya imani tulivu kwa umma. Hasira ni sawa na moto humeza hekima chanya.
Ndugu Bulembo, nimeamua nikupe yangu maono mema, japo wewe umeongea na umma kupitia hekima za andiko lako.
Ndugu Bulembo, umma nao una haki ya Katiba ya nchi na CCM ni mtumishi kwa maslahi sahihi ya jamii na Taifa letu.
Kwa hiyo sasa, wawakilishi wa umma wakipumua chungu-tamu, hekima chanya za kutengua kasoro zitendeke. Nakutakia Kheri kwa mjadala huu, mola ajalie ukunjue sintofahamu.
Ndimi Mzee Shibuda JP.
(RTD MP) Na Mwenyekiti Mstaafu.
Baraza La Vyama Vya Siasa TZ.