Vodacom Tanzania Foundation yatoa msaada wa Kibinadamu kwa waathirika wa Mafuriko Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge (wa pili kulia) akipokea msaada wa kibinadamu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko ya Rufiji na Kibiti wenye thamani ya takribani shilingi 250m uliotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Vyombo vya Habari wa kampuni ya Vodacom Tanzania Annette Kanora (katikati). Wengine pichani kutoka kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald na Meneja Mauzo wa eneo hilo Suleiman Amri na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele (kulia). Msaada huo ulikabidhiwa mwishoni mwa wiki mjini Kibiti.

Related Posts