KALLEIYA AMEHIMIZA KUUNDA KAMATI ZA UCHUMI CCM KATA NA MATAWI ILI KUJIIMARISHA KIUCHUMI

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha April 24

Katibu wa CCM Wilaya Kibaha Mjini , mkoani Pwani, Issack Kalleiya amehimiza kuunda kamati za uchumi kila kata na matawi pamoja na kuanzisha vitenga uchumi ili kukiimarisha kiuchumi.

Wito huo aliutoa alipokuwa kata ya Kongowe ,ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea kata 14 ,yenye malengo wa kujitambulisha kukagua uhai wa Chama na Jumuiya na maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Vilevile aliwaonya wanao wasumbua wenyeviti wa serikali za mitaa ,waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na taribu za CCM ni kuvunja katiba na kanuni za maadili.

Kalleiya alielekeza viongozi wa CCM kuwaunga mkono na kufanya kazi na viongozi waliopo madarakani hadi watakapomaliza muda wao.

Alisisitiza kuongeza kasi ya hamasa kuongeza wanachama wapya kujisajili kielectronic na umuhimu wa kulipa ada ya uwanachama.

“Tuongeze nguvu, wanachama ni mtaji,hatunabudi kuendelea kushawishi ili kupata ongezeko kubwa la wanachama,licha ya wanachama tulipe ada ili kuwa hai,na tuelekeze kujiimarisha kwa kitu kimoja,tuungane,tuache makundi” alisisitiza Kalleiya.

Katibu Kalleiya pia amezungumza na watumishi wa serikali ngazi ya kata na mitaa kusikiliza maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Serikali ya dkt Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini , Silvestry Koka na madiwani wote wa halmashauri Mji Kibaha na wenyeviti wa serikali za mitaa.

Related Posts