Maelfu ya raia Bangladesh wakusanyika kwenye ibada kuomba kupata mvua

Maelfu ya raia wa Bangladesh walikusanyika kuombea mvua siku ya Jumatano katikati ya wimbi kubwa la joto lililosababisha mamlaka kufunga shule kote nchini.

Utafiti wa kina wa kisayansi umegundua mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha mawimbi ya joto kuwa marefu, mara kwa mara na makali zaidi.

Ofisi ya hali ya hewa ya Bangladesh inasema kwamba wastani wa viwango vya juu vya joto katika mji mkuu wa Dhaka katika wiki iliyopita vimekuwa nyuzi joto 4-5 (nyuzi 39-41) juu kuliko wastani wa miaka 30 kwa kipindi hicho.

Waumini wa Kiislamu walikusanyika katika misikiti ya mijini na mashambani kuombea afueni kutokana na joto kali, ambalo watabiri wanatarajia kuendelea kwa angalau wiki nyingine.

“Kuomba mvua ni mila ya nabii wetu. Tulitubu kwa ajili ya dhambi zetu na kuomba baraka zake kwa ajili ya mvua,” Muhammad Abu Yusuf, mhubiri wa Kiislamu ambaye aliongoza ibada ya asubuhi kwa watu 1,000 katikati mwa Dhaka, aliiambia AFP.

“Maisha yamekuwa magumu kutokana na ukosefu wa mvua,” alisema. “Watu maskini wanateseka sana.”

Polisi walisema ibada za maombi ya ukubwa sawa zilifanyika katika maeneo mengine kadhaa ya Bangladesh.

Chama kikubwa zaidi cha Kiislamu nchini humo, Jamaat-e-Islami, kilitoa taarifa kikiwaita wanachama wake kujiunga na ibada ya maombi iliyopangwa kufanyika Jumatano na Alhamisi.

Related Posts