NIDA yapata mafanikio katika miaka 60 ya Muungano

*Ni katika kutoa vitambulisho Kwa idadi kubwa ya wananchi

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa katika miaka 60 Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mamlaka imepata mafanikio ya kutoa Vitambulisho Kwa idadi kubwa.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Godfrey Tengeneza wakati akizungumza kuhusiana mafanikio ya mamlaka hiyo.

Tengeneza amesema kuwa hadi kufikia kutoa Vitambulisho hivyo kulitokana na kuweka mipango mikakati na kuweza kufanikisha hilo.

Aidha amesema kuwa katika utoaji vitambulisho ulihusisha vitambulisho vya Uzawa asili na vitambulisho vya wageni waliopo nchini na kukidhi vigezo vya Ukazi.

Amesema katika kufanikisha hilo ni pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kuweka jitihada katika kuhakikisha wananchi wanapata vitambulisho wakati awali walikuwa wakitumia namba.

Tengeneza amesema katika mipango mikakati ilikuwa ni kuimarisha ofisi katika Wilaya na Mikoa ambapo ndio kumefanya matokeo chanya bila kukutana na changamoto katika mchakato wa vitambulisho.

Hata hivyo katika 60 ya Muungano Mamlaka inaendelea na kusajili kwa mujibu wa sheria na kutambua vitambulisho vinahitajika katika utambuzi mbalimbali kwa wananchi katika upatikanaji wa huduma za kijamii na biashara.

Tengeneza amesema ametoa hofu ya wananchi kuwa kupata kitambulisho cha Taifa ni haki hivyo hakuhitaji kutumia gharama na kinachohitajika ni kukamilisha nyaraka zinazohitaji kutokana na muongozo wa fumu.
 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Godfrey Tengeneza akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na mafanikio katika miaka 60 ya Muungano kwa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Related Posts