Rasmi chanjo ya Saratani kutolewa DSM, Mkuu wa Wilaya anena “maeneo yote watapewa”

Mkoa wa Dar es Salaam umezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo wa Saratani la mlango wa uzazi kwa wasichana mwenye umri kati ya miaka 9 hadi 14 ambapo Wasichana Zaidi ya Laki 150,000 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo mkoani wa Dar es Salaam.

Akizungumzia wakati wa zoezi la utoaji wa Chanjo hiyo mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe, Edward Mpogolo akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe, Albert Chalamila amewaagiza Maafisa Afya wahakikishe maeneo yote yaliyoandaliwa kutolewa huduma hiyo ya chanjo yanafanya hivyo kwa viwango vya juu ili kuwalinda watoto wa kike na saratani hiyo hatari.

Mpogolo amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni lazima iwafikie wanafunzi wanaosoma kwenye shule zote za Msingi na Sekondari sambamba na ambao wanaishi mitaani nao wapate fursa ya kupata chanjo hiyo ili kuwakinga na saratari na mlango wa uzazi.

Related Posts