Yanga SC waingia Mkataba na ATCL, watanufaika hivi

Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Yanga SC leo wameingia mkataba wa miaka miwili wa ushirika na shirika la ndege la Air Tanzania(ATCL).

Katika ushirika huo Klabu ya Yanga italitangaza shirika hilo na watapata punguzo la bei kwa safari zao zote za ndege watakazofanya na shirika hilo.

Mkataba huo wa Yanga na ATCL umesainiwa na Rais wao Hersi Said pamoja na Mkurugenzi wa ATCL Laudslaus Matindi.

“Tumekuwa na ushirika na Young Africans SC kwa muda mrefu sana, lakini kwa sasa tumeona umuhimu wa kuyaweka katika mfumo rasmi. Mkataba huu msingi wake haswa ni mabadilishano ya huduma.

“Ushirika huu faida yake sio tu kwa ATCL bali hata kwa vivutio vyetu vya utalii ambavyo tumekuwa tukivitangaza” Mhandisi Ladislaus Matindi


“Tumesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitangaza Air Tanzania katika kipindi chote hicho. Nasi kama Young Africans SC tuna matumaini makubwa kuwa tutaendelea kunufaika na huduma bora za shirika hili kwa bei punguzo. Tunatambua mchango mkubwa wa ATCL kwa Klabu yetu nasi tunao wajibu wa kuwaunga mkono” Rais Eng. Hersi Said

Related Posts