AIRTEL TANZANIA YAINGIA UBIA NA TADB KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Dinesh Balsingh wakibadilishana mkataba wa kuendeleza sekta ya kilimo na kuwa ya Kidijitali.

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Dinesh Balsingh wakisaini Mkataba wa kuendeleza sekta ya kilimo na kuwa ya Kidijitali.

AIRTEL TANZANIA imeingia makubalino na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kusaini makubaliano (MoU) ya miaka mitatu ikiwa na lengo la kuinua na kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo kwa njia ya mtandao yaani kidijitali.

Makubaliano ya ushirikiano huu kati ya Airtel Tanzania na TADB yanadhamira ya kufanikisha kupanua ushirikiano wa sekta ya kifedha kwa wadau mbalimbali ndani ya sekta kilimo, wakiwemo wakulima, wajasiriamali wadogo vijijini, hasa wanawake na vijana. Ushirikiano wa Airtel na TADB ni moja kati ya juhudi za Airtel Tanzania kuunga mkono serikali katika kuleta matokeo chanya katika maisha ya Watanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka saini makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Dinesh Balsingh, alisema “Airtel kwa kushirikiana na TADB tunadhamira ya dhati ya kusaidia Watanzania kupitia ubunifu katika sekta ya mawasiliano. Hii ni kwakuwa tunaamini wakulima wanastahili kuwa miongoni mwa vikundi vinatakiwa kunufaika na ukuaji wa teknolojia nchini. Hivyo, Ushirikiano wetu na TADB unalenga katika kutatua changamoto zinazowakabili wakulima kwa kutumia bidhaa mbalimbali za kidijitali ambazo zitaibua masoko mapya kwa wakulima mijini na vijijini. Bidhaa hizo zitawezesha uzalishaji wa wakulima na kuongeza mapato yao”.

Balsingh alieleza kuwa ushirikiano wa Airtel na TADB unaungana moja kwa moja na maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ya ukuaji wa sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030. (Chanzo World Economic Forum). ” Na hii inaonesha jinsi kilimo kilivyo muhimu katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watu wamejiajiri katika sekta ya Kilimo.”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege alitoa shukrani zake kwa Airtel Tanzania akisema, ushirikiano wa Airtel na TADB utafungua milango ya fursa katika sekta ya kilimo. Ushirikiano huu utatoa fursa kwa wakulima kujipatia masuluhisho kwenye mahitaji na changamoto wanazokutana nazo katika shughuli zao za kila siku.

“Ubia wa Airtel na TADB unalenga kukuza ukuaji sekta ya kilimo. Ushirikiano huu ni mwanzo wa mabadiliko makubwa yatakayowagusa wakulima wote nchini Tanzania,” alisema Bw. Frank Nyabundege – Mkurugenzi Mkuu wa TADB.

Ushirikiano huu wa Airtel na TADB unakwenda sambamba pia na mikakati ya serikali ya kuunga mkono juhudi za wadau wa kilimo kwa kupambaa na changamoto mbalimbali ndani ya sekta ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima kifedha kama ilivyotajwa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa wadau wa COP28 uliofanyika Disemba 4, 2023. Alisema, “tunatakiwa kubadilika na kufanya kilimo endelevu kwa kuunga mkono ubunifu mbalimbali unaoendana na hali ya sasa.”

Related Posts