GEITA.RC. SHIGELA NA WANANCHI WAKUSANYIKA KUSIKILIZA HOTUBA YA RAIS DKT.SAMIA HASSAN.

Mkuu wa Mkoa wa Geita , Martine Shigela na Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba pamoja na wananchi wa Mji wa Geita wamekusanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Geita katika kufatilia hotuba ya Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuelekea siku ya Muungano inayoadhimishwa kila Mwaka ifikapo April 26.

Akisikiliza hotuba hiyo Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza Maendeleo ya Mkoa wa Geita hasa katika upande wa elimu , Afya na Maji.

Sherehe hizo zimepewa jina la Usiku wa Muungano ambao umeambatana na kupigwa fataki lengo likiwa ni kuashiria amani na upendo na Muungano uzidi kuimarika zaidi.

Sherehe hizo za Muungano Kimkoa zinatarajia kufanyika katika wilaya ya Mbogwe hapo kesho na Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Geita , Hashimu Komba amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa hotuba nzuri kwa watanzania huku akiahidi kuendelea kuchapa kazi na kuendelea kuwatumikia wakazi wa wilaya ya Geita.

Related Posts