MWENGE WA UHURU KUINGIA MKOA WA PWANI APRILI 29

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza  na Waandishi wa Habari  Ofisini kwake leo Aprili  25, 2024 hawapo pichani.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv

MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ametoa ratiba ya kuukimbiza Mwenye wa Uhuru ambao utaingia Mkoa wa Pwani Aprili 29 ukitokea Mkoa wa Morogoro.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano leo Aprili 25 amesema kuwa Mwenge huo wa Uhuru utakimbizwa kwa siku saba.

RC Kunenge amesema kuwa baada ya kuupokea Mwenge wa Uhuru utaanza kukimbizwa Aprili 29 ndani ya Halmashauri ya Chalinze na Aprili 30 utakimbizwa Halmashauri ya Bagamoyo huku Mei mosi utaikimbiza Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Mei mbili utakimbizwa Halmashauri ya Mji Kibaha Mei tatu utakimbizwa Kisarawe, Mei 4 Mkuranga, Mei tano Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Rufiji na Mei 6 utakimbizwa Kibiti huku Mei 7 utakimbizwa Mafia na Mei nane utakabidhiwa Mkoa wa Dar es Salaam.

“Mkoa wa Pwani haturudi nyuma tutakuwa na mipango mizuri zaidi awali ya yote tumegundua changamoto ambazo zimetukabili za mvua hivyo kuna baadhi ya miradi ambayo imebidi tuighairi kutokanaa na mvua.

“Kimkoa tumejipanga vizuri na tunatarajia utakimbizwa katika Wilaya zetu zote tisa pia napenda kuchukua fursa hii kiwaomba wananchi wote wajitokeze kukimbiza Mwenge na kukahikisha tunafanikisha mbio za mwaka huu za mwaka 2024, huku tukitarajia kufumisha upendo,amani utu na heshima.

Amesema pindi mwenge ukikimbizwa Mkoa ni pwani utakua nakauli mbiu za Kuzuia na kuoambana a rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu,jamii iunge jitihada za kutokomeza uonjwa wa UKIMWI, Epuka dawa za kukevya zingatia utu boresha tiba na kinga na mwisho Lishe siyo kujaza tumbo zingatia unachokula,

Ziro Malaria inaanza na mimi chukua hatua kuotokomeza.

Related Posts