Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo Wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) hii ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa umma hasa kwenye vyuo vinavyotoa masomo ya Ununuzi na Ugavi.
Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee amesema Bodi hiyo imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi hiyo ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao pamoja na maadili na miiko ya taaluma hiyo.
Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Jonnes Lugoye ametoa shukrani kwa wafanyakazi wa PSPTB kwa kuweza kufika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.