Ukatili wa kijinsia igeuzwe kuwa ajenda na viongozi wa dini

Kuelekea katika kilele cha miaka 60 ya Muungano viongozi wa dini mkoani Manyara wameoliombea Taifa, Rais Samia Suluhu na serikali yake ili Tanzania iendelee kuwa na amani, upendo na mshikamano.

Viongozi wa dini, watumishi wa umma na wananchi wa mkoa wa Manyara wamejitokeza katika uwanja wa michezo wa Tanzanite Kwaraa wakilenga kumshukuru Mungu kwa mafanikio makubwa ya miaka 60 ya muungano.

Aidha Baadhi ya Viongozi hao wa Dini Wameiomba Serikali kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kero za Maji Migogoro ya ardhi, changamoto ambazo zimekuwa sugu katika Baadhi ya Maeneo

Kwa Upande mwingine Wameiomba Serikali kuangalia Upya namna ya kuboresha sheria za Barabarani na kutoa elimu kwa madereva ili kuzuia Ajali zinazoweza kuepukika

“Serikali iangalie Sana kwa Upya janga linalotokana na ajali linalosababishwa na uendeshwaji hovyo hasa Bodaboda Tumepoteza na tunapoteza Nguvu kazi kubwa Ya Taifa”Alisema Peter Konki -Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim Pentecoste Tanzania

Katika maombi hayo Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Mariam Muhaji ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa viongozi hao wa dini kuendelea kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji ambavyo vimekithiri mkoani humo pamoja na wananchi kuwa na hofu ya Mungu.

Related Posts