Ushirikiano wa Benki ya Stanbic na Ramani waenda kuboresha sekta ya biashara nchini.

Na Mwandishi wetu

Benki ya Stanbic Tanzania na Kampuni ya Ramani zaingia ushirikiano wenye lengo la kimkakati la kuleta mabadiliko katika sekta ya biashara na kuendeleza upatikanaji wa huduma Bora za kifedha hapa nchini.

Akizungumza na waandishi mapema hivi karibuni Mkuu wa Kitengo cha biashara wa benki ya Stanbic Tanzania Fredrick Max katika hafla fupi ya utilianaji wa Saini wa makubariano ya ushirikiano wa kibiashara.

Aidha Ushirikiano na Ramani ni zaidi ya biashara na ni ushirikiano wa kimkakati ambao unaahidi kubadilisha na kuboresha namna biashara zinavyofanyika nchini Kwani utaunganisha nguvu na maono ya pande mbili na kusaidia mahitaji ya kifedha ya wasambazaji wa ndani na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa ” Amesema Max

Hata hivyo Lengo kuu ni kutoa fedha kwa wasambazaji na wauzaji, ili kuboresha usimamizi wa ugavi kwa wasambazaji, na wafanyabiashara wa bidhaa kubwa kama nchini ambalo itawezesha usimamizi bora wa manunuzi, udhibiti wa hisa, na ufuatiliaji wa mauzo ya kidijitali, katika kuimarisha michakato ya biashara na miamala ya kifedha.

Kwa upande wake Iain Usiri, mkurugenzi mtendaji wa Ramani, amefurahishwa na ushirikiano huwo kwa kuwa utaongeza huduma za kifedha na na kurahisisha mambo mbalimbali katika sekta ya biashara hapa nchini.

“Tunafurahi kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania. Ushirikiano huu utarahisisha na kuimarisha usimamizi wa wasifu wa mikopo, na kukuza huduma za kifedha. Tunaleta mabadiliko chanya katika kuendesha biashara, na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha.” Amesema Laini Usiri.

Mafanikio ya ushirikiano huu yatapimwa na uandikishwaji wa wafanyabiashara 100 katika mwaka wa kwanza, na mipango ya kukuza ufikiaji kwa kiasi kikubwa, ili kufikia biashara zaidi nchini Tanzania.

Fredrick Max, Mkuu wa kitengo cha biashara Stanbic Bank (Kulia) akiwa na Iain Usiri Mkurugenzi mtendaji wa Ramani (Kushoto) wakizindua rasmi ushirikiano wa taasisi hizo mbili za kifedha.

Takwimu za mitandao ya kijamii, ukuaji wa kifedha, na viwango vya kuandikisha wateja, zitatumika kama viashiria muhimu vya mafanikio na ufanisi wa muunganiko huu.

Ushirikiano kati ya Benki ya Stanbic Tanzania na Ramani, unatengeneza kiwango kipya cha ushirikiano katika sekta ya kifedha na teknolojia, huku ukionyesha matumaini makubwa katika kuboresha jinsi biashara inavyofanywa na kusaidiwa kifedha nchini Tanzania.

Kupitia hatua hii, mashirika yote mawili yanathibitisha azma ya kuchochea ukuaji wa kiuchumi, na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.

Related Posts