Mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Ndg. Salum Mwalim akitoa salam kwa niaba ya uongozi wa Baraza hilo wanaomaliza muda wao wakati wa mkutano wa uchaguzi wa viongozi wapya wa Baraza hilo uliofanyika leo tarehe 24 April 2024 Zanzibar katika ukumbi wa Spring Hall, uliopo Madinat Al Bahr Hotel. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi
Na: Frank Shija, ORPP
BARAZA la Vyama vya Siasa limeafiki kutoa pongezi za dhati kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kuimarisha Demokrasia nchini kwa kuboresha Baraza la Vyama vya Siasa nchini.
Hayo yamebainishwa na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ndg. Salum Mwalimu wakati akitoa salaam kwa niaba ya Baraza hilo kabla ya uchaguzi wa viongozi wapya wa Kamati ya Uongozi ya baraza hilo uliofanyika tarehe 24 April 2024 Zanzibar katika Ukumbi wa Spring Hall Madinat Al Bahr Hotel.
“ Kuna wakati tumemuweka Jaji Mutungi kwenye kitimoto lakini ni wahakikishie tuendelee kuweka imani kwenye kamati ya uongozi, mtakumbuka hatukuwa na Bajeti kwenye Baraza la Vyama vya Siasa lakini chini ya kamati yenu tumefanyakazi kubwa sana mpaka leo msije mkasema na mpigia mtu kampeni lakini ndani ya miaka miwili tuna bajeti yetu iliyopitishwa Bungeni,na tumeandaa mikutano miwili mikubwa ambayo imeleta tija kubwa kwa Taifa letu, yote haya ni nia njema ya Serikali kuhakikisha Demokrasia inazidi kuimarika” Alisema Salum Mwalimu.
Aliongeza kuwa kuundwa kwa Kikosi kazi ni zao la Baraza la Vyama vya Siasa kilichotokana na Baraza hili kupitia Kamati ya Uongozi na Sekretarieti chini ya Jaji Francis Mutungi na tumefanikiwa kuandaa mikutano miwili ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Bara na Visiwani.
“Mheshimiwa Jaji amesema kabla ya kikao cha Baraza kutakuwa na vikao vya Kamati jambo ambalo tumelipigania muda mrefu sana hii inaonyesha Dhahiri nia njema ya Serikali kuhakikisha Demokrasia inaimarika, mtaona kwa mara ya kwanza juzi kuna kadude kameingia kwenye vyama vyetu kuhakikisha tunasafisha karoti na kuhakikisha akaunti ipo active, kazi ile imefanywa kwa wivu mkubwa na kamati ya uongozi na kupokelewa na Jaji Mutungi na Sekretairieti na wakaitekeleza ndani ya muda mfupi, na mheshimiwa Jaji kuna jambo alilisema ambalo kilikuwa kilio chetu cha muda mrefu cha kamati kukakaa kabla ya Baraza” aliongeza Mwalimu.
Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi alisema kuwa wakati wanapanga mikutano ya Baraza la Vyama vya Siasa vitatanguliwa na vikao vya Kamati za Baraza la Vyama vya Sias ambavyo vipo kikanuni kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
“Ebu tulionyeshe Taifa ili kuwa tuliopo hapa tuna haki yakukutana na kujadiliana, jana nilitakakusema kwamba Kamati ya uongozi haiwezi kukaa kabla Kamati hazijakaa, kiutaratibu zinatakiwa zile kamati kukaa arafu wenyeviti wanakuja kutuambia yaliyojiri kutoka katika kamati zao” Ailisema Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi aliongeza kuwa lengo la kuwa na vikao vya kamati kabla ya kikao cha Baraza ni kuhakikisha kuwa masuala yote yanayojadiliwa katika Baraza yawe yametoka chini kwenyevyama husika ikiwa ni njia sahihi ya kujenga na kuhimarisha Demokrasia na umoja wa kitaifa.
“ Sasa tunatakiwa tuboreshe taarifa zetu ambazo hwa wawakilishi wanaokuja kwenye Baraza zinakuwa zimeanzia chini kutoka kwenye vyama vyetu zilitwe kwenye kamati ya uongozi mwisho kwenye baraza ata mtu akisema Msajili mwenyewe ni Jaji mimi mwenye nakuwa na vitu ambavyo vimetokana na mfumo mzima ambao tumetokanao kwenye Baraza la vyama vya Siasa”. Aliongeza Jaji Mutungi.
Akizungumzia chimbuko la Baraza la Vyama vya Siasa Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa Chama cha Mbizu Ndg. Vuai Ali Vuai Mwafaka wa Oktoba wa 2001 baina ya CCM na CUF ulioibuka na muafaka wa kuanzishwa kwa chombo ambacho kitawakutanisha wadau wa siasa kwa lengo la kuwa na jukwaa la kukutanisha wadau ili kujadiliana namna ya kuendesha siasa za Tanzania.
“Baraza limetoka mbali lakini chanzo cha Baraza hili litokana na mazungumzo yaliyokuwa yanendele kwa muda mrefu ya Makatibu wa Kuu wa CUF na CCM baadaye zikaundwa kamati wajumbe wakateuliwa kutoka vyama hivyo wakatengeneza document iliyojulikana MUAFAKA wa Oktoba 2001 lengo lake lilikuwa kujenga umoja baada ya maelewano na kuafikiana hatimaye kiundwe chombo kimoja kitakachowakutanisha viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa ili wapate mahali pakuzungumzia masuala ya kisiasa kwa mustakabari wa Maendeleo ya watanzani”. Alisema Mhe. Vuai.
Mkutano huo wa Baraza la Vyama vya Siasa umefanyika Visiwani Zanzibar kwa Siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 ambapo ulitanguliwa na Kikaocha Kamati ya Uongozi lkilichafanyika tarehe 22 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Bunge Zanzibar na kufuatiwa na mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ulioshirikisha Makatibu wa Vyama wasiokuwa wajumbe wa Baraza na wawakilishi wa wanawake na kisha kuhitimishwa na mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Kamati za Uongozi wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Spring Hall uliop katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Zanzibar.