Fundi atelekeza mradi na bweni wilayani Bukombe mkoani Geita

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita Imebaini kucheleweshwa kwa ujenzi wa mradi wa Mabweni 03 katika shule ya Sekondari Bukombe yenye thamani ya Shilingi Milioni 390.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita , Azza Mtaita wakati akiwasilisha kwa wandishi ripoti ya robo ya mwaka ambapo amesema mradi huo umecheleweshwa kwa kipindi cha Miezi mitatu huku sababu zikitajwa ni Fundi wa bweni moja kukimbia mradi.

Aidha TAKUKURU imeshauri ili kuondokana na changamoto hizo wameshauri katika Mikataba waweke vipengele vinavyowabana Mafundi wanaochelewesha kazi na wale wanaokimbia kazi.

Mtaita amesema katika kipindi cha January 2024 hadi Machi 2024 TAKUKURU mkoa wa Geita iliweza kutekeleza kazi 14 na kero 84 zilizoibuliwa ambapo katika kero hizo , Kero 28 zimepatiwa Majibu na Kero 56 na zilizo wasilishwa idara huska ili zipatiwe ufumbuzi .

Ikumbukwe kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita imefanikiwa kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo 24 yenye thamani ya shilingi Bilioni 27,155,743,651. Miradi 13 haikuwa na Mapungufu makubwa na miradi 11 ndio ilikuwa na Mapungufu.

Related Posts