Marufuku kutumia baiskeli ya mwanafunzi kwenda kunywea pombe

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amepiga Marufuku Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa kike waliokabidhiwa Baiskeli na Shirika la Plan International zitakazo kwenda kusaidia kupunguza Changamoto ya Umbali mrefu kuacha tabia ya kuzichua Baiskeli hizo na kwenda kuzitumia kwa Matumizi mengine ikiwemo kunywea Pombe

Marufuku hiyo imepigwa wakati alipokuwa akikabidhi Baiskeli 550 kwa wanafunzi wa Mkoa wa Geita na kigoma zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 180 huku akiwataka wanafunzi kutoa taarifa kwa wazazi watakaokwamisha mwanafunzi kushindwa kwenda shule kwa tabia ya kwenda kunywea Pombe Baiskeli hiyo.

“Kwa swala la Utunzaji ni swala letu sote watoto wa kike wanafunzi ukisumbuliwa nyumbani wewe peleka taarifa kwa Mwalimu wako Baiskeli ipo lakini Mama amekuwa ni Mkorofi kila siku anataka yeye ndio achukue afate ndizi akauze sokoni kwa Baiskeli ya shule haikubariki tutoe Taarifa kwa walimu , ” RC.Shigela.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi ya Plan International Tanzania Laurent Wambula amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza kubuni Miradi mbalimbali kwa lengo la kuisaidia Jamii pamoja na wanafunzi wanaotoka katika Mazingira Magumu hasa kwa Mkoa wa Geita.

” Tumekua na Miradi inayohusiana na Afya Tumejenga vituo vya Afya Tumejenga ufahamu juu ya Mambo mbalimbali yanayohusiana na afya ya Mtoto afya ya vijana walio katika umri balehe pamoja na Vijana lakini pia kwa kushirikiana na kamati mbalimbali za Mtakua tumeshirikiana na kuhakikisha kwamba mtoto au haki zake zinalindwa , ” Mkurugenzi wa Miradi ya Plan International Tanzania.

Prudence Temba ni Makamu Mwenyekiti wa Balaza la Madiwani Halmashauri ya Mji Geita akimwakilisha Mwenyekiti amelipongeza Shirika hilo huku akikiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali kwa wanafunzi wanaoishi katika Mazingira Magumu kushindwa kumaliza Masomo yao na badala yake kukomea njiani.

Related Posts