Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema baadhi ya maeneo katika mikoa 16 ya Tanzania bara na visiwa na Unguja na Pemba zitashuhudia mvua kubwa leo Ijumaa, Aprili 26, 2024.
Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simivu, Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa na visiwa vya Unguja na Pemba.
Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 26, 2024 na TMA huku ikiweka angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili.
Upepo huo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba).
“Athari zinazoweza kujitokeza, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini,” imeelezwa na TMA.
Kwa siku zilizobaki kuanzia Aprili 27 hadi Aprili 30, TMA imetoa tahadhari ya ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mita mbili.
Upepo huo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) na ukanda wa ziwa Nyasa (Mikoa ya Songwe, Njombe na Ruvuma).
Aprili 28, 2024, TMA imesema kutakuwa na upepo mkali unaoziDi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.
“Tahadhari hiyo ni kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikon ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) na ukanda wa ziwa Nyasa (Mikoa ya Songwe, Njombe na Ruvuma,” imeandikwa.
Aprili 29, TMA imesema upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayouzidi mita mbili itakumba baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aprili 30, Upepo mkali wa kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili pia itashuhudiwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).