MAMBA WATISHIA USALAMA WA WANANCHI WA KATA YA RUVU.

NA WILLIUM PAUL, SAME. 

MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wananchi wa kata ya Ruvu kuwa makini na maji yanayotapakaa katika maeneo hayo kutoka mto Ruvu kutokana na maji hayo kuja na mamba ambao wanaweza kuleta madhara kwao. 

Mkuu huyo wa wilaya pia amewaagiza Tarura kufika katika kata hiyo na kuona jinsi watakavyoweza kufungua njia ambapo kwa sasa maji yametapakaa kila mahali hali inayiwalazimu wananchi kutumia mitumbwi kutoka kwenda kutafuta mahitaji yao.

Kasilda amewataka kuacha kufanya shughuli za uvuvi wa samaki kiholela katika maeneo hayo kwani mamba hao wamekuwa wakiwakimbiza wananchi ambapo mpaka sasa Mwananchi mmoja ameshauwawa. 

Kwa upande wake, Diwani wa kata ya Ruvu, Yaigongo Mrutu amesema kuwa eneo kubwa la kata hiyo limezungukwa na maji yakiwamo mashamba ambapo kwa sasa wananchi hawajui hatima yao. 


Related Posts