Maonesho ya Kwata ya Kikundi cha Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania kutoka Zanzibar Maarufu kama Askari wa Tarabushi wakionesha Maonesho mbalimbali ya aina ya Kwata tangu kipindi cha utawala wa Sultan na kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Askari hao walijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uvaaji wa Kofia zao za Tarabushi. Onesho hilo lilifanyika katika kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024
Askari wa Kikundi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akishuka kwenye Helikopta kwa ajili ya kwenda kuelezea namna mbalimbali za kwata na mapigano ya mjini wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.