BARAZA la Michezo Nchini (BMT) La ahidi kushirikiana bega kwa bega na Shirikisho la Mbio za Magari (AAT) Kuhakikisha wadau wanaunga mkono mchezo huo.
Akizungumza na Wadau na Wachezaji wa Mashindano ya mbio za magari wakati wa Kugawa tuzo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la michezo (BMT) Neema Msitha amesema amefarijika kuona Shirikisho la Mbio za Magari (AAT)Wamekumbuka na kuwakutanisha wachezaji wa Mashindano haya ya magari na kufanya hivyo ni kuwatia Moyo ili kufanya vizuri zaidi hivyo nafasi ya ushindani itaendelea kuwepo.
Aidha amesema Lengo la Serikali ni Kuona michezo inaendelea kupaa zaidi endapo mtu mmoja mmoja hatotambua nafasi yake .
“Zinapokuwepo Medali au nishani inawasaidia wachezaji hao kuendelea kufanya vizuri ndani na nje ya nchi na kuitambulisha nchi ya Tanzania katika michezo.
Pia ametoa wito kwa Shirikisho la mbio za magari (AAT) kutafuta wadau ambao watawekeza katika mchezo huo na kuendelea kuibua vipaji mbalimbali kama michezo mengine.
Aidha Kwa Upande wake Rais wa Shirikisho la mbio za Magari (AAT) Nizar jivan amesema Chama hicho Kitaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuendelea kuwepo kwa Mafunzo ya Usalama Barabarani Nashuleni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
“Chama hichi kimekuwa kikishirikiana kwa karibu na Serikali na tumekuwa tukijitolea kwa kuwafata Wanafunzi mashuleni kuwapa mafunzo ya usalama barabarani na kuboresha miundombinu ikiwemo kuweka vivuko barabarani maeneo karibu na shule za Misingi.”
Hata hivyo amesema tuzo hizo zitaendelea kutolewa kila mwaka ili kuwatia moyo wachezaji hao wa mbio za Magari nchini sanjari na Mafunzo mbalimbali yanaendelea kutolewa kwa lengo la usalama barabarani kwa wachezaji hao.
Pia ametoa wito kwa washini wote waliofanikiwa kupata Tuzo kuendelea kushiriki mchezo huo kwa usalama kwani imejengeka desturi kuwa mchezo ni hatari na unapoteza maisha kwa haraka zaidi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la michezo (BMT) Neema Msitha akikabidhi Kikombe Kwa Mshindi dereva bora Mr.Birdi katika hafla ya Tuzo za Usiku wa Mabingwa wa Mashindano ya mbio za Magari Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) akizungumza na Wadau wa Mashindano ya Mbio za Magari wakati wa Tuzo zao Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wachezaji hao kutafuta wadhamini ili kuendeleza mchezo huo
Mwenyekiti wa Shirikisho la mbio za magari (AAT) Satinder bird akiwa na Washindi wa Mashindano ya Mbio za Magari kutoka Klabu mbalimbali sherehe iliyofanyika Jijini Dar es Salaam