PURA yaibuka kinara tuzo za ushiriki wa watanzania

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi zinazoshirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kutekeleza masuala ya local content.

Kufuatia ushindi huo, PURA imekabidhiwa tuzo maalum wakati wa hafla ya kuhitimisha Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati iliyofanyika Aprili 28, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Akitoa maelezo ya Kamati ya kujitegemea iliyoundwa kuratibu mchakato wa tuzo hizo, Mwenyekiti wa Kamati Bw. Christopher Mushi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI alieleza kuwa ushindani ulifanyika kwa kuzingatia vigezo vya kila kundi.

“Kila kundi lilitakiwa kuwa na washiriki wasiopungua watano na washindi wa kila kundi walitakiwa kupata alama za ufaulu zisizopungua asilimia hamsini” alifafanua Bw. Mushi.

Tuzo zilikabidhiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuhitimisha Kongamano hilo.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko (kushoto) akikabidhi tuzo kwa PURA baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi zinazoshirikiana na NEEC kutekeleza masuala la local content. Anayepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PURA ni Bw. Charles Nyangi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau kutoka PURA. Tuzo hiyo imetolewa wakati wa halfa ya kuhitimisha Kongamano la Nne la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi kimkakati iliyofanyika Aprili 28, 2024

Related Posts