Na Mary Margwe, SIMANJIRO.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Fakii Raphael Lulandala amesema katika kipindi Cha Serikali ya awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya shughuli nyingi na kubwa na kuiletea Tanzania Mafanikio makubwa ya Maendeleo katika Sekta karibia zote.
Akizungumza juzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Qeen Sendiga aliyekua mgeni rasmi kwenye Kilele Cha Maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofayika kimkoa katika Wilayani Simanjiro, Mkuu huyo amesema Tanganyika na Zanzibar inasheherekea miaka 60 ya Muungano nchi ikiwa na Mafanikio ya MIUNDOMBINU ( barabara )
Amesema katika kipindi Cha Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Serikali imefanya mengi na makubwa katika jamii katika Sekta na elimu Kuna madarasa mengi ya Rais Samia na yenye ubora mkubwa, kwenye Sekta ya afya karibia kila Tarafa ina Kituo cha afya, Hospitali za Wilaya na hospitali za Mkoa.
” Tukisema tuorodheshe mambo mengi na makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake Cha miaka mitatu, muda hautatosha” amesema DC Lulandala
Aidha Lulandala amesema pamoja na kwamba bado kuna uhitaji wa maji lakini Mamlaka za maji zinafika mahali husika kupeleka maji ” Tunasheherekea miaka 60 ya Muungano tukiwa tumeshuhudia Mafanikio / Maendeleo makubwa ” amesema Mkuu huyo.
Amesema Wana Manyara Wana furaha kuwa na wanaunga mkono juhudi zinazofanywa Serikali ya awamu ya sita katika kuiendeleza ,kudumisha na kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
” Sisi kama Wana Manyara tuna furaha kubwa sana na tunafunga mkono kabisa juhudi zinazofanywa na Serikali yetu katika kuiendeleza, kudumisha na kuimarisha Muungano wetu, pia tunaendelea kuwa wasimamizi Wazuri wa shughuli zote za miradi ya Maendeleo zinazotekelezwa na kusimamiwa na Serikali hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha ulinzi, Usalama Amani vinaendelea kuwepo miongoni mwa wananchi wetu” amefafanua Mh.Lulandala.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Maryam Muhaji ameitaka jamii kuhakikisha wanaimarisha Muungano huo, pamoja na kukemea vitendo vya Ukatili wa Kijinsia unayoendelea katika Mkoani humo.
Kufuatia kuwepo kwa vitendo hivyo ndani ya Mkoa huo amewaomba viongozi wa Dini katika Makanisa na misikiti suala la Ukatili wa Kijinsia iwe ndio agenda ya kukemea ukatili wa kijinsia.
” Wana Manyara ni wazuri sana isipokua lakini tunaharibiwa na huu ushwerati ambao umetutawala kwenye suala Zima la Ukatili, hivyo Viongozi wa Dini niwaombe kulitenda hili Kwa haraka zaidi ili liweze kuwa na mwitikio mzuri kwa jamii.
Naye Katibu wa Siasa , Itikadina na Mafunzo Mkoa wa Manyara John Nzwalile amesema zipo faida nyingi za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hivyo kuwaomba Watanzania kutoruhusu watu kuubeza Muungano huo.
Nzwalile amesema Muungano ndio maisha, Mafanikio yote yanayoonekana yamefanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si vinginevyo.
” Naomba Watanzania wasiruhusu watu kuubeza Muungano wetu huu, Muungano wetu huu ndio maisha yetu, Mafanikio yote unayoyaona yamefanywa na Serikali yetu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwasababu ya utulivu, amani na Usalama iliyowekwa na viongozi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ” amefafanua Nzwalile.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Wilaya ya Simanjiro Anna Shinini amesema Muungano huo umeendelea kuwaunganisha akina mama Kwa Umoja wao na kuwapa nguvu, ujasiri mkubwa wa kufanya kazi hususani kupitia nafasi ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kama mwanamke shupavu, Mahili katika kuliongoza Taifa Kama Rais
” Siku ya leo na Mimi kama Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro namuunga mkono mama yetu Mchapakazi Mh. Samia Suluhu Hassan ambaye ni mwanamke aliyetujengea ujasiri mkubwa na sisi tunamuumga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kumtia moyo katika Utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku, amesema Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Simanjiro
Aidha Shinini amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo ya asilimia 10 iliyokua ikitolewa katika kila Halmashauri hapa Nchini kupitia mapato yake ya ndani, ni mikopo iliyokuwa na msaada mkubwa sana kwa walengwa katika kuwaondoa katika wimbi la u amaskini na kuwainua kiuchumi.
” Nimefurahi sana leo kusikia ile mikopo ya asilimia 10 imerudi, kwani ilikua ndio nguzo muhimu ya kumkomboa mwanamke, vijana na Watu wenye ulemavu na hatimaye kuwakomboa kwenye wimbi la umaskini, kwani mikopo ya nje ya Serikali baadhi imekua ni mikopo kandamizi Kwa kuwa na riba kubwa iliyowapelekea hata baadhi yao kufilisiwa mali zao kwa kushindwa kurejesha marejesho.
Aisha SHININI amesema Mikopo hii ilishakuwepo ambapo Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu walikua wakinufaika nayo kwani Serikali imekua ikitoka mikopo hiyo hiyo bila riba ili kuwawezesha kuinua uchumi na hivyo kuwawiaburahisi kuwaletea Maendeleo ya haraka, ukilinganisha na hiyo mikopo mingine.
” Sasa wanaendelea kupata mikopo, tunamshuku sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo hii ambayo itawasaidia kuwainua kiuchumi na hatimaye kuweza kuondokana na umaskini, kikubwa ni umaminifu wa kuchukua fedha na kurudisha”
Kufuatia hilo pia amewataka wanaochukua mikopo kuweza kuhakikisha mikopo wanayoichukua inawanufaisha kisawa sawa ikiwa ni sambamba na kurudisha fedha hizo Kwa wakati ili iliwe kuwasaidia na wengine
Aidha amewataka wanawake pamoja na wananchi wote Kwa ujumla kuhakikisha wanamuunga mama mkono kwasababu Muungano wetu ni kioo, ni dira ndani ya nchi yetu ndio inayotuonyesha tumetoka wapi, tuko wapi na tunatarajia kufika wapi, na hivyo Rais Samia anatupa nguvu zaidi kuweza kufanya kazi ndani ya Taifa letu.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM] Wilaya ya Simanjiro Timothy Ngoyai Mollel amesema Muungano umeendelea kuimarisha Umoja na ushirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar.
” Kupitia Muungano pia tumeendelea kujifunza kazi kubwa zinazotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa Utekelezaji wa Miradi mingi na mikubwa hapa chini, lakini pia hata katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro nayo umeendelea kupata mingi na mikubwa.