KOCHA Msaizidi wa Simba, Seleman Matola ameachiwa msala wa kuiongoza timu hiyo kati-ka mechi zilizosalia na Ligi Kuu Bara ikiwamo wa keshokutwa dhidi ya Namungo, baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha kuamua kuachana na timu hiyo akitoka kuipa Kombe la Muungano lililofanyika Zanzibar.
Benchika aliyetambulishwa na Simba Novemba 28 mwaka jana, anaondoka sambamba na wa-saidizi aliokuja nao, akiwamo kocha msaidizi, Farid Zemiti na yule wa utimamu wa mwili (Fitness Coach) Kamal Boudjenane ikiwa amei-tumikia timu hiyo kwa muda wa siku 157 tu akiitwaa nayo taji hilo moja la Muungano.
Wakati tukienda mitamboni, Simba ilikuwa iki-jiandaa kutoa taarifa za kuachana na Benchikha kama ambavyo Mwanaspoti la jana liliwadokeza kwa kichwa cha habari kisemacho ‘ANASEPA’ wakati timu ikiwa imewasili jijini Dar es Salaam na kuunganisha safari ya kwenda Lindi kuiwahi Namungo huku Matola akiachiwa kila kitu.
Simba itakuwa mgeni wa Namungo katika mechi itakayopigwa kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Majaliwa, mjini Lindi na timu itakuwa chini ya Matola atakayesaidiana na ko-cha wa makipa, Dani Cadena aliyewahi kuinoa Azam FC kabla ya kutua Msimbazi.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kililidokeza Mwanaspoti kuwa, Benchikha na wasaidizi alikuja nao wote wameondoka kikosini na jukumu la kuinoa timu lipo kwa Ma-tola na Cadena wakati viongozi wanajipanga ku-saka kocha mpya.
Inaelezwa kuwa, mara baada ya timu kufika bandarini jijini Dar es Salaam ikitokea Zanzibar ilikoenda kucheza Kombe la Muungano na ku-litwaa kwa kuifunga Azam kwa bao 1-0, kocha Benchika alipanda gari ndogo kwenda hotelini ambako anaishi huku timu ikipanda basi tayari kwa safari kuifuata Namungo.
“Timu inaondoka na kocha msaidizi Matola sa-fari inaunganishwa hakuna kwenda kambini wa-la wachezaji kuruhusiwa kwenda makwao baada ya kutua bandarini, tumepanda basi moja kwa moja kuanza safari ya kwenda Lindi,” kilisema chanzo hicho kutoka Simba kilichoongeza;
“Kocha mkuu hatakuwa sehemu ya mchezo huo, kwani tayari ameagana na wachezaji na benchi la ufundi mara baada ya kutwaa Kombe la Muungano nafikiri sasa timu itakuwa chini ya Matola.”
Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam.
Simba ilitwaa taji la Muungano lililoshirikisha timu nne tu likiwa ni la sita baada ya awali ku-litwaa mwaka 1993, 1994, 1995, 2001 na 2002 na Benchikha ameondoka akiwa amewapa taji hilo pekee, huku Ngao ya Jamii iliyotwaliwa na timu hiyo Agosti 13 mwaka jana ikiwa chini ya kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’.
Simba inaachana na Benchikha kwa kile Mwa-naspoti inachofahamu kwamba ni kutokana na matatizo ya kifamilia kwao Algeria, akiwa ame-dumu kwa siku 157 tangu alipomuajiri Novem-ba 24 na kumtambulisha siku nne baadaye akichukua nafasi ya Robertinho
Robertinho aliondoka Novemba 7, mwaka jana ikiwa ni muda mchache tangu timu hiyo ilipofungwa mabao 5-1, dhidi ya Yanga na kuvunja rekodi ya kutopoteza tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipofungwa na Azam FC bao 1-0, Oktoba 27, 2022.
Tangu atambulishwe, Benchikha ameiongoza timu hiyo katika michezo 21 katika mashindano yote ikiwemo ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Ligi ya Muungano iliyorejea mwaka huu.
Katika Ligi Kuu Bara ameiongoza katika michezo 11 ambapo kati ya hiyo ameshinda sita, sare mitatu na kuchezea kichapo mara mbili hu-ku akifunga jumla ya mabao 18 na kuruhusu nyavu za kikosi hicho kutingishwa mara nane tu hadi sasa msimu huu.
Ni michezo miwili tu ya Ligi Kuu Bara ambayo Benchikha hakuiongoza Simba ambayo ni dhidi ya Coastal Union ambayo timu hiyo ilishinda mabao 2-1 (Machi 9, 2024) na ushindi wa 3-1 mbele ya Singida Fountain Gate uliopigwa Machi 12, mwaka huu.
Sababu za kukosekana kwake katika michezo hiyo ni kutokana na kwenda kwao Algeria kwa ajili ya kushiriki kozi ya ukocha ya siku tano.
Katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ali-iongoza katika michezo saba ambapo kati ya hiyo alishinda miwili, sare miwili na kupoteza mitatu huku kiujumla Simba ikifunga jumla ya mabao manane na kuruhusu nyavu zake kuting-ishwa mara nne tu nyavuni.
Michuano mingine ni katika Kombe la Shiriki-sho la Azam (ASFC) ambapo Benchikha alijiku-ta akitolewa mapema tu hatua ya 16 Bora dhidi ya Mashujaa ya Kigoma baada ya timu hizo kufungana bao 1-1, kisha kuaga kwa penalti 6-5.
Katika Ligi ya Muungano iliyorejea mwaka huu baada ya kusimama kwa miaka 22, Benchikha aliiongoza Simba katika mechi mbili na kushin-da 2-0 dhidi ya KVZ kisha 1-0 akiifunga Azam kwenye fainali.
Kiujumla katika michezo hiyo 21, Simba ikiwa chini ya Benchikha imefunga jumla ya mabao 30 huku ikiruhusu kufungwa mabao 13.