Habari Matukio kwa Picha: Rais Samia akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika April 29, 2024 Admin Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Nchi mbalimbali mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA nje ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Nairobi nchini Kenya Aprili 29, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi nchini Kenya leo Aprili 29, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan akifuatilia hutoba zilizokuwa zinawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya leo Aprili 29, 2024. Related Posts Habari KONA YA MSTAAFU: Kila mtu ni mstaafu mtarajiwa anayepaswa kutetea wastaafu January 17, 2025 Admin Habari Wafanyakazi wanavyoweza kudhibiti maradhi ya kisukari January 17, 2025 Admin