https://p.dw.com/p/4fI8S
Kulingana na maafisa wa afya wa Wapalestina mmoja wa watoto waliouawa katika mashambulizi hayo ya usiku wa kuamkia leo alikuwa wa siku 5 tu.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani John Kirby amesema juhudi za kufikia makubaliano ya usitishaji vita kati ya Israel na kundi la Hamas kwa wiki sita bado yanaendelea.
Haya yanajiri huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akianza ziara yake ya saba katika Mashariki ya Kati tangu vita vya Israel na Hamas kuanza zaidi ya miezi sita iliyopita.