Akizungumza mbele ya umati wa viongozi, wabunifu, na wageni waliohudhuria mkutano huo, Waziri Nnauye alisisitiza maono yanayojadiliwa na washiriki kuhusu matumizi ya teknolojia za kidijitali kama kichocheo cha maendeleo ya Afrika katika enzi hizi za kidijitali.
Akisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika Mkataba wa Kidijitali wa Kimataifa na Akili Mnemba (AI), Waziri Nnauye amesisitiza umuhimu wa kuelekeza juhudi kuendeleza ajenda ya kidijitali ya Afrika.
Akizungumzia maelezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Eliud Owalo kuhusu Mkataba wa Kidijitali wa Kimataifa kwa mtizamo wa Bara la Afrika, Waziri Nnauye alilenga mazungumzo yake kwenye jukumu na umuhimu wa miundombinu ya kidijitali kama msingi wa maendeleo ya kisasa. Alihimiza umuhimu wa kukabiliana na mbinu inayozingatia uvumbuzi pamoja na usimamizi wenye ufanisi ili kuhakikisha ukuaji endelevu katika eneo la kidijitali.
Katika mkutano huo, washiriki walijikita katika majadiliano yenye kulenga kuandaa tamko la pamoja linalothibitisha azma ya Afrika kwa Mkataba wa Kidijitali wa Kimataifa na usimamizi wa Akili Mnemba (AI). Waziri Nnauye alielezea umuhimu wa kuwa na mpango wa vitendo utakaoboresha sera, kuimarisha miradi ya ujenzi wa uwezo, na kuchochea ushirikiano wa kimataifa ili kugeuza ahadi kuwa matokeo yanayoweza kuhisika yanayowanufaisha mataifa katika bara zima.
Waziri Nnauye aliwahimiza washiriki wote kutafakari ufahamu muhimu ulioshirikishwa na njia za ushirikiano zilizopatikana wakati wa mkutano huo. Alisema Tanzania na mataifa mengine ya Afrika yanatakiwa kuelekea kwenye mageuzi ya kidijitali na maendeleo endelevu utakaonesha uwezo wa bara la Afrika kutumia nguvu ya teknolojia kwa maendeleo ya pamoja ya watu wake.
Mkutano wa “Connected Africa 2024” unatumika kama jukwaa muhimu kwa viongozi kukutana, kubadilishana mawazo, na kupanga mkakati kuelekea mustakabali wa teknolojia kwa Afrika, huku hotuba ya Waziri Nnauye ikiwa ni uthibitisho wa dhati wa azma ya Tanzania ya kusonga mbele katika sekta ya TEHAMA.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akibadilishana mawazo na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika waliofika kushiriki Kongamano la Connected Africa Summit 2024 linalofanyika katika Ukumbi wa Uhuru Garden jijini Nairobi, Kenya leo Aprili 22, 2024.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akisalimiana na Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto aliyewasili kwenye hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Connected Africa Summit 2024 linalofanyika katika Ukumbi wa Uhuru Garden jijini Nairobi, Kenya leo Aprili 22, 2024.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akiwasili katika Ukumbi wa Uhuru Garden uliopo katika jiji la Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Connected Africa Summit 2024 linalofanyika leo Aprili 22, 2024.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akibadilishana mawazo na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika waliofika kushiriki Kongamano la Connected Africa Summit 2024 linalofanyika katika Ukumbi wa Uhuru Garden jijini Nairobi, Kenya leo Aprili 22, 2024.