NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
WASOMI wametakiwa kuchukua jukumu na kuendeleza tafiti ambazo zitachapishwa katika kanzi data za kimataifa kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuufikia Ulimwengu mzima ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Ameyasema hayo leo Aprili 30,2024 Jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Saalaam, Prof. Rwekeza Mukandala wakati wakiadhimisha miaka 50 ya Jarida lake la The African Review lililojizolea umaarufu duniani kwa kuandaa mijadala ya kisomi kuhusiana na siasa za Afrika, Maendeleo pamoja na masuala ya Kimataifa.
Aidha Prof. Mukandala amesema Jarida hilo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa kipindi cha Ukombozi wa bara la Afrika hasa Afrika ya Kusini ambayo bado ilikuwa ikikaliwa na mkoloni ambapo walikuwa wakipitia mateso mbalimbali na udhalimu wa kibeberu.
Kwa Upande wake, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Utafiti) Prof.Nelson Boniphace amesema watu wanaweza kujaribu kuandika kwa mfumo wa akili bandia (artificial intelligence) na kudanganya ambapo wamejizatiti kwa kutoa elimu kwa wahariri wao,ilikubaini machapisho hayo endapo itatokea udanganyifu.
“Lakini tuna Teknolojia ya kuweza kuyabaini Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kimewekeza kwa kutoa elimu kwa wahariri wake ili kuyatambua majarida hayo na kulinda viwango visishuke” amesema Prof. Boniface.
Aidha Prof. Boniphace ameeleza kuwa wamewekeza katika majarida yao mengine ambapo wamefanya usajiri na kanzi data Elsevier ambapo kufikia mwezi wa Saba 2024 watakua na mamlaka ya ya kufikiaji Jarida lao katika kanzi data hiyo katika nyanja mbalimbali zaSayansi ya jamii,uhandisi,na biashara.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. Wiliam Anangisye amesema kuwa tukio hilo kubwa la kihistoria linaacha alama kubwa nchini na kuipatia jamii ya wanazuoni fursa ya kujifunza tangu kuchapishwa kwa Jarida hilo mwaka 1971.
Aidha Prof. Anangisye amesema Jarida hilo la The African Review ni jarida la kwanza nchini ambalo limefikia Viwango vya kimataifa kwa kupatikana katika kanzi data ya kimataifa ya Scoopers ambapo imekuwa ikipokea makala mbalimbali za watu kutoka nje ya nchi.
Vilevile, Mhariri Mkuu wa Jarida la The African Review,Prof. Alexander Makulilo amesema mwaka 2019 chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kiliingia mkataba na wachapishaji wanaopatikana nchi ya uholanzi ilikujjenga miundo mbinu ya kufanya chapisho hilo kwenda kimataifa Jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
“Chapisho lilikua linatoka Mara mbili kwa mwaka na kwa Sasa linatoka Mara tano,na mwakani tunatarajia litatoka Mara sita lakini pia ubora wake umezidi kwenda mbele, kwasababu sasa hivi makala zaidi ya asilimia 70 zinakataliwa kwa sababu ya ubora wake baada ya kufanyiwa Tathimini tunasema hapana, kwahiyo tutatakua tunapokea asilimia 15 pekee kutunza ubora wake.”Prof.Makulilo amesema.
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilitarajia kufanya hafla hiyo miaka mitatu iliyopita ambapo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO -19 ilizuia kufanyika kwa tukio hilo,ambalo limefanyika leo Aprili 30,2024 na kuinua hisia tofauti kwa wasomi wapya.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. Wiliam Anangisye akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya Jarida lake la The African Review lililojizolea umaarufu duniani kwa kuandaa mijadala ya kisomi kuhusiana na siasa za Afrika, Maendeleo pamoja na masuala ya Kimataifa.
Mhariri Mkuu wa Jarida la The African Review,Prof. Alexander Makulilo akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 50 ya Jarida lake la The African Review lililojizolea umaarufu duniani kwa kuandaa mijadala ya kisomi kuhusiana na siasa za Afrika, Maendeleo pamoja na masuala ya Kimataifa.